Sunday, February 26, 2017

PSPTB YATOA MAFUNZO YA UNUNUZI NA UGAVI KWA WAFANYAKAZI WA MFUKO WA MISITU TANZANIA (TFF)


9
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akifunga mafunzo ya Ununuzi na Ugavi wa Umma yaliyokuwa yakitolewa kwa wafanyakazi wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TFF) ambayo yalifanyika kwa siku nne kwenye Shule ya Sekondari ya wasichana mjini Kibaha mkoani Pwani.
Wataalam wa bodi hiyo walitoa mafunzo kuhusu sheria ya ununuzi wa Umma na kanuni zake pamoja na mabadiliko ya mwaka 2016, Aidha mafunzo yayo yalijadili taratibu za kuandaa nyaraka za zabuni, taratibu za uchambuzi wa zabuni na uidhinishaji wa zabuni kwa ujumla wake.
Washiriki wa mafunzo hayo walikumbuswa majukumu na mipaka ya utendaji wao kama inavyoelekezwa kwenye sheria na ununuzi wa Umma, Washiriki hao pia walikumbushwa na kujadili kwa kina wajibu wao katika kuandaa na kutekeleza mikataba ya ununuzi kwani  ndiyo nguzo muhimu katika kutekeleza mikataba ya ununuzi wa vifaa , huduma na kazi za majenzi
Kaimu Mkurugenzi huyo aliwakumbushwa wataalamu hao wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TFF) kuwa ni wajibu wao kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kuiweka bodi ya (PSPTB) katika sifa na yenye manufaa kwa taifa.
2
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akizungumza na Amosi Kasinza Afisa Mkuu wa Utafiti na Ushauri PSPTB wakati alipowasili shuleni hapo kwa ajili ya kufunga mafunzo hayo.
3
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) Bw. Paul Bilabaye akifunga mafunzo akitoa mada katika mafunzo yaliyotolewa na bodi hiyo kwa wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka Mfuko wa Misitu (TFF).
5
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo hayo.
6 7
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akizungumza na Amosi Kasinza Afisa Mkuu wa Utafiti na Ushauri PSPTB wakifuatilia mafunzo hayo.
8  Amosi Kasinza Afisa Mkuu wa Utafiti na Ushauri PSPTB akitoa mada  mafunzo hayo.10
Patricia Manonga Afisa Miradi wa Mfuko wa Misitu akishukuru Uongozi wa bodi ya (PSPTB) kwa kutoa mafunzo hayo.11
Dk. Tuli Msuya Katibu Tawala wa Mfuko wa Misitu Tanzania TFF akishukuru kwa wataalam wa mfuko huo kupata mafunzo hayo ambayo ni muhimu sana kwao kama wataalam wa Ununuzi na Ugavi wa Umma.12
Mwenyekiti wa Bodi ya Tenda ya Mfuko wa Misitu Tanzania Bw.Kelvin Mtei akitoa neno la shukurani kwa bodi ya (PSPTB) kwa kuwapa mafunzo hayo.
13
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hao mmoja wa washiriki wa mafunzo.
14
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifunga mafunzo hayo.
15
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi pamoja na baadhi ya  wataalam wa Bodi ya PSPTB wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.

No comments :

Post a Comment