Wednesday, February 1, 2017

NBC YAWAPONGEZA WAFANYAKAZI WAKE BORA


1
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Corporate, Mariam Kombo (kushoto), akionyesha cheti alichotunukiwa mara baada ya kutangazwa meneja bora wa mwaka 2016 kutokana na utendaji wake mahiri katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
2
Meneja wa Kanda wa Benki ya NBC James Ndimbo (kushoto), akionyesha cheti mara baada ya kutangazwa meneja bora wa kanda wa mwaka 2016 kutokana na utendaji wake mahiri katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi na kulia ni mkuu wa idara ya Biashara NBC Elvis Ndunguru. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
3
Meneja wa amana za wateja NBC, Dorothea Mabonye (kushoto), akikabidhi kombe la ushindi kwa Meneja wa Tawi la NBC Sea Cliff baada ya tawi hilo kuibuka kidedea katika kutoa huduma za kibenki kwa wateja wa akaunti ya malengo kwa mwaka 2016 . Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
4
Mkuu wa idara ya mikopo binafsi wa NBC, Andrew Lyimo, akimkabidhi kikombe cha ushindi meneja wa tawi la Samora, Faustina Maeda (katikati) aliyeibuka kidedea katika utoaji wa mikopo kwa watu binafsi katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora kwa mwaka 2016. Kulia ni Mtenya Cheya, meneja mikopo kwa watu binafsi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
5
Mkuu wa Idara ya Mauzo wa NBC, Mongateko Makongoro (mwenye suti nyeusi) akipiga picha ya pamoja na washindi wa tuzo ya utoaji wa mikopo binafsi walioingia kwenye Kundi la Watu Mashuhuri wa NBC lijulikanalo kama ‘ ‘Kundi la Shilingi Billioni Moja’. Tuzo hizo zilitolewa kwenye sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora kwa mwaka 2016. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
6
Mkurugenzi wa Huduma Reja Reja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi (wa tatu kushoto), akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi bora waliofanya vizuri katika mwaka 2016 walio chini ya kurugenzi yake, katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora kwa mwaka 2016. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

No comments :

Post a Comment