MFUKO WA LSF WATOA MSAADA WA LAPTOP KWA WASAIDIZI WA KISHERIA KWA JAMII
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen (kulia)
akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa
msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo
ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na
Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka
Uingereza. Kushoto ni Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk
akishuhudia.[/caption]
MFUKO wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) umekabidhi laptop 170 kwa
asasi mbalimbali zinazotoa msaada wa kisheria kwa wananchi wahitaji
katika mikoa anuai nchini Tanzania.
Akizungumza kabla ya kukabidhi vitendea kazi hivyo kwa wawakilishi wa
mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa wa kisheria, Mjumbe wa Bodi ya
LSF, Dk. Benson Bana aliwataka sema shirika hilo linaamini zitatumika
katika kutatua changamoto anuai kwa asasi husika ikiwa ni chachu ya
kuongeza ufanisi kwa kazi zao.
Laptop hizo 170 zimekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa
Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen huku akizitaka asasi hizo
muhimu kuendelea kuisaidia jamii inayoitaji msaada wa kisheria popote
walipo kwani zipo familia hasa wajane wanaitaji na wanashindwa namna ya
kupata.
LSF ni mfuko huru wa msaada wa kisheria unaotoa msaada kwa mashirika
watoa msaada wa kisheria, kitaasisi na kiufundi ili kuongeza uwazi na
uwajibikaji katika sekta ya sheria chini ya ufadhili wa Shirika la
DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID la Uingereza.
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
No comments :
Post a Comment