Wednesday, February 22, 2017

KAMPUNI YA JAPAN YAONYESHA NIA YA KUIUZIA TBL VIFUNGASHIO VYA KISASA


1
Meneja wa Kiwanda cha   Bia Tanzania (TBL Group )   Calvin Martin (wa pili kulia) Mhandisi wa mitambo wa TBL Group Chrispine Christopher (Kulia) pamoja na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa mambo ya nje  wa kampuni hiyo Edith Mushi , wakisikiliza maelezo ya Meneja Mkuu wa  Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni ya  Toyo Seikan Group Holdings Ltd ya Tokyo Japan( General manager of Business Development)   Yashimasa Ito (kushoto).
2
Meneja wa Kiwanda cha   Bia Tanzania (TBL Group )   Calvin Martin (kushoto)  akiwapa maelezo baadhi maofisa wa Kampuni ya  Toyo Seikan Group Holdings Ltd ya Tokyo Japan inayojihusisha na uzalishaji wa vifungashia vya bia ,kutoka kulia ni Afisa wa JICA  mhandisi Patrick Marwa  na Meneja Mkuu wa  Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni ya  Toyo Seikan Group Holdings Ltd ya Tokyo Japan   Yashimasa Ito
3
Maofisa kutoka Kampuni ya  Toyo Seikan Group Holdings Ltd ya Tokyo Japan inayojihusisha na uzalishaji wa vifungashio  wakimsikiliza kwa makini Meneja Uzalishaji wa TBL Group ,(Packaging Manager) Patel Kilovela  (Kulia) wakati walipotembelea kiwandani hapo
4
Meneja wa Kiwanda cha   Bia Tanzania (TBL Group )   Calvin Martin (kushoto) na  mhandisi wa Mitambo wa TBL Group Chrispine Christopher (Kulia)  wakionyeshwa na Meneja Mkuu wa  Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni ya  Toyo Seikan Group Holdings Ltd ya Tokyo Japan (Yashimasa Ito (katikati) moja ya vifungashio vianavyotengenezwa na kampuni yake.  
Kampuni ya Toyo Seikan Group Holding Ltd kutoka nchini Japan imeonyesha dhamira ya kuwekeza nchini kwa kuzalisha vifungashio vya vinywaji vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya maofisa wa kampuni hiyo wako nchini kufanya utafiti wa masoko .

 Ujumbe wa maofisa wake umetembelea kiwanda cha bia Tanzania (TBL)  kwa ajili ya kujifunza jinsi kinavyofanya kazi ikiwemo kuonyesha vifungashio vilivyotengeneza kwa teknolojia ya kisasa ambavyo kampuni hiyo hiyo inazalisha.
Meneja Mkuu wa  Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni  hiyo , Yashimasa Ito,ambaye ameongoza ujumbe huo ameelezwa kuvutiwa na hatua kubwa ya kiteknolojia ambayo kampuni ya TBL  imefikia katika mchakato wa kuzalisha bia na alisema kuwa  wanayo yadhamira ya kuwekeza nchini na kutengeneza vifungashio kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi iwapo watakuwa na uhakika wa kupata masoko ya kutosha.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa kiwanda cha TBL cha Ilala,Calvin Martin,aliueleza ujumbe wa maofisa wa kampuni hiyo mikakati mbalimbali inayotekelezwa na kampuni kuhakikisha inaenda sambamba na teknolojia za kisasa zinazotumiwa na viwanda vyote vikubwa vya kutengeneza bia na vinywaji vingine duniani.
“Tumevutiwa na dhamira yenu ya kuwekeza nchini kwa kuwa kampuni yetu iko mstari wa mbele kwenda sambamba na teknolojia na ndio maana viwanda vyetu vinashikilia rekodi ya kuwa viwanda bora barani Afrika pia bidhaa zetu zinatamba katika masoko ya kimataifa”.Alisema Calvin.

No comments :

Post a Comment