Kamishna Jenerali wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya hafla fupi ya utiaji
saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo
cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro.
Hafla hiyo imefanyika leo Februari 24, 2017 katika Ofisi za Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya
Mkulazi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF, Bw. Nicander
Kileo (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(kulia) kwa pamoja wakisaini Mkataba wa Makubaliano(Memorundum of
Understanding) kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na
ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro. Hafla hiyo
ya utiaji saini imefanyika leo februari 24, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa(kulia) na Kaimu Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya Mkulazi ya
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF, Bw. Nicander
Kileo(kushoto)wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya hafla fupi ya
uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa
kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza
Mbigiri – Morogoro.
Maafisa Waandamizi wa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF wakifuatilia hafla ya uwekaji saini
wa Mkataba wa Makubaliano hayo kama inavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii wa PPF, Bw. William Erio akizungumza katika hafla fupi
ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa
kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza
Mbigiri – Morogoro.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza wakishuhudia uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano hayo kama
inavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF,
Prof. Godius Kahyarara akizungumza katika hafla fupi ya uwekaji saini
wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi
ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha
miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro.
No comments :
Post a Comment