Monday, February 27, 2017

Halmashauri Nchini Zaagizwa Kuwasilisha Taarifa Kuhusu Maendeleo ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Nchini.


hal1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara katika Halmashauri nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati.
hal2
hal3
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
hal4
Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Kamati ya Uongozi ya MKURABITA na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
hal5
Watendaji kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miji Dkt. Mkuki Hante pamoja na Mkurugenzi wa Utawala kwa Serikali za Mitaa Bibi. Miriam Mmbaga wakifuatilia mjadala wakati wa kikao baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na MKURABITA kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo leo Jijini Dar es Salaam.
hal6
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akipokea taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha rasilimali na biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati leo Jijini Dar es Salaam.
hal7
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akisoma taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha rasilimali na biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9 nchini mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati(hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.
hal8
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala mara baada ya  mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya hiyo Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Na: Mpiga Picha Wetu.
……………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija – MAELEZO.
27/02/2017
Kufuatia kusuasua kwa utekelezaji na maendeleo ya Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara Serikali imeziagiza Halmashauri zote nchini ambazo zimefikia na mpango huo
kuwasilisha taarifa rasmi.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Boniphace Simbachawene katika kikao baina yake na wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA kilichofanyika Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Simbachawene amesema kuwa TAMISEMI ni mdau muhimu katika Mpango huo wa urasimishaji wa rasilimali hivyo ujio wa kamati hiyo kutaka kushirikiana na Tawala za Mikoa ni jambo jema.
“Binafsi ni muumini wa muda mrefu wa mpango huu wa urasimishaji, niseme tu mmechelewa kuja sehemu husika kwa bila dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi kufanikiwa kwa mpango huu itakuwa ni adithi sasa tutaenda pamoja ili kiutimiza azma ya mpango huu,”alisema Simbachawene.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Kapteni wa Jeshi Mstaafu John Chiligati amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa Halmashauri zaidi ya 100 nchini mpaka sasa utekelezaji wa mpango huo umezifikia takribani Halmashauri 52 na Miji 9 tu hivyo kasi yake bado hairidhishi.
Aliongeza kuwa changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa mpango huo ni Halmashauri kuuona mpango huo kama hawahusiki nao hali inayopelekea kushindwa kuendelea pindi mwakilishi wa Mkurabita atakapo ondoka katika eneo husika.
Chiligati amesema kuwa baada ya kubaini changamoto hiyo waliamua kuwa na makubaliano maalum na TAMISEMI juu ya utekelezaji wa pamoja wa mpango huo jambo ambalo wanaendelea kulifanyia kazi.

No comments :

Post a Comment