Mkurugenzi wa Friedkin
Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (wa tatu kulia) akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia) shehena ya mifuko
3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa
shule za sekondari wilayani Meatu. Kampuni hizo Mwiba Holdings na
Tanzania Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 ikiwa ni
msaada. Wengine ni viongozi mbalimbali walioshiriki katika tukio hilo.
Mkurugenzi wa Friedkin
Conservation Fund (FCF), Pratik Patel akizungumza katika tukio la
kampuni hiyo kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni
jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani
Meatu. Kampuni hizo yaani Mwiba Holdings pamoja na Tanzania Game
Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 kama msaada.
Mkurugenzi wa Friedkin
Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (kulia) akimtamkia Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) kuwa mbali na kampuni hiyo kutoa
mifuko 3000 ya saruji kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani
Meatu. Wataongeza msaada wa mabati 1000. Wengine ni Miss Universe
Tanzania 2016/17, Jihan Dimack (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa FCF,
Pratik Patel (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo.
Na Mwandishi Wetu, Simiyu
KAMPUNI kitalii zilizo chini ya
Friedkin Conservation Fund (FCF) Tanzania iliyowekeza katika pori la
Makao wilayani Meatu na Maswa Mkoani Simiyu imechangia mifuko 3000 ya
saruji na mabati na 1000 kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani
humo.
Misaada hiyo yenye thamani ya
zaidi ya sh milioni 70 imetolewa na kampuni hizo ikiwa ni kuunga mkono
mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli
kuendeleza elimu ya hasa katika maeneo ya wafugaji ambako kampuni hizo
zinafanya shughuli za uwindaji wa kitalii.
Kampuni zilizokabidhi misaada hiyo
juzi katika sherehe zilizofanyika mjini hapa ni pamoja na Mwiba
Holdings na Tanzania Game Trackers ambazo kwa pamoja zimetoa saruji hiyo
yenye thamani ya sh milioni 48 na mabati yakiwa na thamani ya sh
milioni 25.
Vifaa hivyo vya ujenzi vitatumika
kujenga vyumba vya madarasa na mabweni kwa ajili ya shule zitakazotumiwa
na watoto wa jamii za wafugaji zinazoishi jirani na maeneo ya shughuli
za uwindaji wa kitalii wilayani Meatu katika mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony
Mtaka (kushoto) akifurahia tamko la Mkurugenzi, Abdulkadir Mohamed
(hayupo pichani) kuahidi kuongeza msaada wa mabati 1000 huku Miss
Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack akikabidhiwa kipaza sauti
kurudia kauli ya neema za mabati 1000 toka FCF.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu
(aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi
shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni ya FCF
kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka pamoja na Miss Universe Tanzania 2016/17,
Jihan Dimack.
Akizungumza kabla ya kumkabidhi
mchango huo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, wakati wa hafla
iliyofanyikia katika viwanja vya stendi Mjini Mwanhnuzi, Mkurugenzi wa
Kampuni hiyo Abdulkadir Mohamed alisema kuwa mchango huo unatokana na
kuanzishwa kwa mfuko uwekezaji katika pori hilo.
“Tunatoa msaada huo ikiwa ni
kuunga mkono Serikali yetu ya awamu ya tano katika jitihada za
kuimarisha sekta ya elimu nchini,na tumeanza kuwasaidia wananchi
tunaoshirikiana nao katika shughuli za uhifadhi na huu ndio mwanzo wa
kuendeleza ushirikiano huu ikiwa ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii,”
alisisitiza Mkurugenzi huyo
Alisema kuwa pamoja na kuchangia
misaada hiyo,kampuni yake imekuwa ikitoa misaada katika vijiji tisa
vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi za Wanyama Pori Makao (WMA) na ranchi ya
Mwiba hasa katika kusaidia uboreshaji wa huduma za jamii na hasa elimu.
“ Mpaka sasa Kampuni kupitia
makampuni yake matatu tayari wamechangia kiasi cha sh Milioni 3000 kwa
vijiji tisa pamoja na vingine 15 vinavyopakana pori hilo, ambapo shule,
zahanati, pamoja na vituo vya maendeleo vimejsengwa katika vijiji hivyo
kwa kushirikiana na halmashauri” Alisema Mohamed.
Aidha, aliongeza kuwa mchango huo
umechangiwa na mafanikio mazuri ya shughuli za utalii zinazoendelea
katika maeneo hayo na uwekezaji wa kampuni hiyo wilayani humo, huku
akibainisha kuwa shughuli hizo zinazidi kupanda kila mwaka wilayani humo
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiongozana na wageni wake katika hafla hiyo.
Miss Universe Tanzania 2016/17,
Jihan Dimack akijitambulisha katika hafla ya FCF kukabidhi shehena ya
mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kusaidia ujenzi wa shule za
sekondari wilayani Meatu.
Mkurugenzi huyo aliahidi kuwa
kutokana na kuimarika kwa shughuli hizo na kuwepo kwa mazingira mazuri
ya uwekezaji,hasa ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wananchi, hasa
wavijiji vinavyopakana na pori hilo, wamepanga kuongeza uwekezaji wao
kwa dola za kimarekani milioni 100.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti
maalum Mkoa (CCM) Leah Komanya alipongeza mchango wa mwekezaji huyo,
huku akiunga mkono kwa kuchangia mabati 50 kwa ajili ya ujenzi wa
mabweni shule ya sekondari Makao.
“ niwaombe hawa wawekezaji wetu
wasichangie kwenye vijiji hivyo tisa peke yake, bali wachangie hata
kwenye kata nyingine za wilaya yetu ambayo ipo chini sana kielimu ili
kila mwananchi atambue mchango wao, na niwapongeze kwa kuunga mkono
ujenzi wa shule hasa mabweni kwa watoto wa kike” Alisema Komanya
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
akizungumza kabla ya kupokea msaada huo, alimtaka Mkurugenzi huyo ambao
alidai kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro ya kila mara kati ya wananchi
na kampuni hiyo ili kurejesha imani ya kuendelea kushirikiana na
wawekezaji hao.
Mbali na hilo Mtaka alipongeza
Kampuni hiyo kwa mchango wake, huku akielelekeza saruji hiyo pamoja na
mabati vitumike kwa ajili ya kujenga mabweni katika shule za sekondari
zinazopakana na pori hilo.
Mtaka aliwataka wawekezaji hao
kuwa karibu na wananchi kwa kushirikiana na watendaji wa halmashauri na
alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuwapatia
kiwanja cha kujenga ofisi ili iweze kuratibu kwa karibu ushirikiano huo
na wananchi.
Kwa sasa mgogoro uliodaiwa kuwapo
kati ya mwekezaji huyo na wanakijiji wa Makao, umemalizika baada ya
msuluhishi aliyeteuliwa na pande zote mbili, Jaji Thomas Mihayo, kutoa
uamuzi hivi karibuni baada ya walalamikaji kushindwa kuwasilisha utetezi
wao kwa wakati.
Hata hivyo, taarifa zimeeleza
kwamba hali hiyo imetokana na kurejea kwa mahusiano kati ya pande hizo
mbili na kuonekana njia bora zaidi ya kusuluhisha migogoro ni mazungumzo
yasiyo na gharama zinazoweza kuigharimu serikali ya kijiji na wilaya.
No comments :
Post a Comment