Wakati
filamu zitakazochuana katika tuzo za mwaka huu za Africa Magic Viewers’
Choice(AMVCAs) zikitangazwa, filamu kutoka Tanzania zimeibuka katika
Makundi matatu tofauti kitendo kinacholeta matumaini ya kuona makubwa ya
watanzania kuwika kwenye tuzo hizo zitakazofanyika katika jiji la Lagos
nchini Nigeria mnamo mwezi Machi 2017
Filamu za Kitanzania zinawika
katika kundi la Filamu Bora kabisa Afrika Mashariki ambapo kati ya
filamu tano zilizoteuliwa, tatu ni za kitanzania ambazo ni “Aisha” ya
Amil Shivji,
“Naomba Niseme” ya Staford Kihore, na “Homecoming” ya Seko
Shamte.
Kundi jingine ambalo filamu za
Tanzania zimejitokeza ni lile la Filamu Bora za lugha ya Kiswahili
ambapo tamthilia ya “Siri ya Mtungi” awamu ya pili ya John, Louise na
Jordan Riber imeteuliwa kushiriki
Kwenye kundi kubwa la Sinema Bora
kabisa barani Africa mwaka 2016, sinema mbili kati ya sita zilizomo
katika kundi hilo ni za Tanzania ambazo ni “Aisha” ya Amil Shivji na
“Naomba Niseme” ya Staford Kihore.
Upigaji wa kura kupendekeza
washindi unaendelea hadi februari 24 ambapo utafungwa rasmi na hafla ya
kutangaza washindi itafanyika tarehe 5 Machi 2017. Upigaji kura
unafanyika kwa njia ya mtandao na
pia mpigakura anaweza kutembelea www.africamagic.tv au www.dstv.com ambapo ataweza kupelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa kupigia kura.
Akizungumzia tuzo hizo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, amewasihi
watanzania kupiga kura kwa wingi ili kuwawezesha washiriki wetu kuibuka
washindi. Amesema kwakuwa washiriki ni wengi na wanatoka nchi mbalimblai
kote Afrika, ni uzalendo pekee wa kuwapigia kura watanzania wenzetu
ndio utakaowahakikishia ushindi.
“Sasa Ni Zamu yetu” alisema
Maharage na kuongeza “Kitendo cha kazi za hawa watanzania kuingia kwenye
mchuano, kinamaanisha kazi zao zina ubora unaokubalika, hivyo inabidi
tuwaunge mkono kwa kuwapigia kura nyingi kadiri iwezekanavy. Watanzania
watambua kuwa sasa ni zamu yetu, na sisi tuuonyeshe ulimwengu kuwa
tunaweza” alisema.
Tanzania ina rikodi nzuri kwenye
tuzo hizi kwani msimu uliopita filamu ya Kitendawili ya Richard
Mtambalike ilinyakua tuzo ya filamu bora tya lugha ya Kiswahili wakati
Elizabeth Michael ‘Lulu’ alivuma katika tuzo hizo katika filamu yake ya
Mapenzi iliyoteuliwa kuwa filamu bora kabisa Afrika Mashariki.
Africa Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA) inafanyika kila mwaka na inaandaliwa na Multichoice
Africa ikiwa na lengo la kutambua na kuthamini mafanikia makubwa katika sekta ya filamu na televisheni
kulingana na uchaguzi wa watazamaji.
No comments :
Post a Comment