Ijumaa Februari 24,2017
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imezikutanisha Asasi za Kiraia
zilizopo katika manispaa hiyo kwenye semina ya siku moja iliyolenga
kuzijengea uwezo ili ziweze kutekeleza vyema shughuli zao katika
kuwaletea maendeleo wananchi.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mgeni rasmi katika semina hiyo
ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika
manispaa ya Shinyanga alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro.
Akizungumza wakati wa kufungua
semina hiyo Matiro amezitaka asasi za kiraia (NGO’s,CBO’) kuepuka kuwa
sehemu ya kushiriki uovu katika jamii wakitumia mwamvuli wa asasi na
kuzitaka kuepuka kuilaumu serikali badala ya kuishauri pale inapokosea.
“Serikali inatambua kazi
nzuri zinazofanywa na asasi za kiraia katika kuisaidia jamii,nyinyi ni
sehemu ya serikali,mnafanya kazi pamoja na serikali kuisaidia
serikali,serikali yetu haiwezi kufanya kila kitu,hivyo haipendezi
kuilaumu serikali,ishaurini pale mnapoona mambo hayaendi sawa”,amesema
Matiro.
“Pia msiwe na usiri katika
shughuli zenu maana zipo asasi zinaingia kimya kimya katika jamii,kabla
ya kuanza kutekeleza mradi jitambulishe katika jamii,elezeni mnafanya
nini pia itatusaidia kujua asasi ipi inafanya nini hali ambayo
itawezesha kupungua kwa idadi ya asasi zinazofanya shughuli moja katika
eneo moja”, ameongeza Matiro.
Naye Mkurugenzi wa manispaa ya
Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi amesema asasi za kiraia
zinatakiwa kuwajibika kwa serikali hivyo zinatakiwa kuwa zinatoa taarifa
serikalini kuhusu shughuli wanazofanya.
Miongoni mwa mada zilizotolewa
katika semina hiyo ni pamoja na sheria za uendeshaji wa asasi za
kiraia,taratibu za uendeshaji wa asasi za kiraia,namna ya kuandaa andiko
la mradi na masuala yanayohusu rushwa.
Mwenyekiti wa semina hiyo
Mchungaji Dkt. Meshack Kulwa kutoka TCCIA Shinyanga akimkaribisha
mgeni,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ili afungua semina
hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo ambapo
alisema serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na asasi za kiraia na
ipo tayari kushirikiano na asasi yoyote katika kuwaletea maendeleo
wananchi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini.Kulia ni Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na viongozi wa asasi za kiraia katika manispaa ya Shinyanga
Naibu meya wa manispaa ya
Shinyanga Agnes Machiya akizungumza ukumbini.Kulia ni Mkurugenzi wa
manispaa ya Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi
Mkurugenzi wa manispaa ya
Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi akizungumza katika semina hiyo
ambayo imekutanisha viongozi mbalimbali wa asasi za kiraia katika
manispaa hiyo
Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa manispaa ya
Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi akisisitiza asasi za kiraia
kushirikiana na serikali katika kuiletea maendeleo jamii
Afisa Uchunguzi Mwandamizi
kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa
Shinyanga Alice Mazoko akitoa mada kuhusu masuala ya rushwa ambapo
alizitaka asasi hizo kujikita katika malengo yao badala ya kugeuka
kichochoro cha kuchuma pesa zisizokuwa halali (rushwa).
Afisa Uchunguzi Mwandamizi
kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa
Shinyanga Alice Mazoko akisisitiza juu ya umuhimu wa asasi za kiraia
kuepuka vitendo vya rushwa katika shughuli zao.
Lubumba Masebu kutoka asasi ya
vijana ya Youth Development Organisation (YUDEN) akichangia hoja wakati
wa semina hiyo ambapo alisema asasi nyingi hazifanikiwi kutokana na
jamii kukosa elimu na kushindwa kuelewa malengo ya miradi husika
Mchumi wa manispaa ya Shinyanga,Alex Mpasa akitoa mada kuhusu namna ya kuandaa andiko la mradi
Mchumi wa manispaa ya
Shinyanga,Alex Mpasa akiendelea kutoa mada.Kulia ni katibu wa chama cha
watu wenye ualbino Lazaro Nael akimsaidia mawasiliano kwa njia ya ishara
mmoja wa washiriki mwenye ulemavu wa kusikia (asiyesikia)
Mwezeshaji akitoa mada ukumbini
Washiriki wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini….
Semina inaendelea
Washiriki wakiwa ukumbini
Semina inaendelea
Semina inaendelea
Viongozi wa asasi za kiraia wakiwa ukumbini
Mwezeshaji akitoa mada kuhusu sheria za uendeshaji wa asasi za kiraia
Afisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Salome Komba akitoa mada kuhusu taratibu za uendeshaji wa asasi za kiraia.
No comments :
Post a Comment