Saturday, February 25, 2017

BODI YA UNUNUZI NA UGAVI WA UMMA (PSPTB) YAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI NA MAADILI KATIKA CHUO CHA (CBE)


1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya  Ununuzi na Ugavi wa Umma PSPTB Bw. Godfred Mbanyi , akifungua  semina ya mafunzo ya uongozi  na madili kwa wanafunzi wa  chuo cha Biashara cha  (CBE) kilichopo jijini Dar es salaam kwa lengo la kupata viongozi  wenye maadili kazini na wenye kufuata kanuni na taratibu za Ununuzi na Ugavi wa Umma.
Semina  hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE)  ambapo jumla ya wafunzi 45 walishiriki katika katika mafunzo  hayo ya Ugavi na Ununuzi wa Umma.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (PSPTB) Bw.  Godfred Mbanyi amesema , lengo la kuanzisha mafunzo hayo ni kutaka kuwajengea uwezo katika utendaji wa kazi wenye ubunifu, maadili na Uadilifu ili kuijengea heshima taaluma ya Ununuzi na Ugavi wa Umma, lakini pia kupata viongozi wenye kufuata misingi ya taaluma kwa ujumla wake , Kulia katika picha ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB)
1
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo ya Uongozi yaliyotolewa na Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB )Zuhura Sinare Muro akizungumza wakati alipokuwa akitoa mada katika mafunzo hayo yaliyofanyika leo kwenye chuo cha Biashara CBE.
2
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia mafunzo hayo.
3
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo ya Uongozi yaliyotolewa na Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB )Zuhura Sinare Muro akifafanua jambo kwa wanafunzi hao
4
Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB)na Afisa Mwandamizi wa  Masoko  na Mahusiano Bi. Shamim Mdee wakiwa katika mafunzo hayo.
5
Baadhi ya wakufunzi wa mafunzo hayo wakifuatilia jambo.
6
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya  Ununuzi na Ugavi wa Umma PSPTB Bw. Godfred Mbanyi akimsikiliza Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB)wakati alipokuwa akitoa shukurani zake mara baada ya Kaimu Mkurugenzi huyo kufungua semina hiyo
7
Baadhi ya wanafunzi wakiuliza maswali katika semina hiyo.
8 4
Baadhi ya maofisa wa PSPTB wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa kwa wanafunzi katika semina hiyo.

No comments :

Post a Comment