Baadhi ya wakazi wa Njombe Mjini wamiwa wanamsikiliza waziri Mkuu Kassm Majaliwa katika maeneo ya Wikichi Mjini Njombe
Waziri mkuu Majaliwa akizungumza na wakazi wa njombe Maeneo ya Hospitali ya Mkoa wa njombe Mtaa wa Wikichi Njombe Mjini.
Wziriri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha chai cha Kibena
WAZIRI
Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa ameahirisha ziara yake mkoani
Njombe ambapo ameelekea jijini Dar es salaam ambako anatarajia kumpokea
Rais wa Uturuki ambaye anakuja hapa nchini kwa ziara ya kikazi Ziara
yake inatarajiwa kuendelea januari 25 kwa siku tatu.
Waziri mkuu amekuwa mkoani Njombe kwa siku tatu ambapo amepita katika halmashauri tatu za mkoa huo kabla ya kuahirisha ziara hiyo na kurejea jijini Dar es Salaam kwa majukumu mengine ya kiutendaji ziara yake mkoani Njombe ilikuwa ya siku sita na kuzitembelea halmashauri zote za mkoa huo.
Waziri
mkuu Juzi aliwaaga viongozi wa mkoa wa Njombe na kuelekea jijini Dar Es
Salaam katika viwanja vya ndege mkoani Iringa huku akitarajia kulejea
tena mkoani humo Januari 25 na kumaliza ziara yake baada ya siku tatu.
Akirejea
Njombe atatembelea halmashauri ya wilaya ya Njombe na kutembelea
kiwanda cha chai na kuzungumza na wakulimqa wa zao hilo, kasha
kuzungumza na wakazi wa Mji wa Njombe baadaye kwenda wilayani Ludewa
ambako pia atakutaa na wakazi wa Mundini na Liganga kutako tarajiwa kuwa
na migodo ya makaa yam awe na Chuma.
Mkuu
wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka akizungumza na Nipashe
kuhusiana na kuahirishwa kwa ziara hiyo alisema kuwa waziri mkuu alikuwa
mkoani humo kwa siku tatu ambapo ameahilisha kuendelea na ziara na
kasha kulejea tena Januari 25.
Alisema kuwa waziri mkuu anaelekea jijini Dar es Salaam kwa kuwa nchi itakuwa ikipokea ugeni wa Rais wa Uturuki ambaye anafanya ziara yake hapa nchini ambapo baada ya ziara ya Rais Huyo Waziri mkuu watalejea Mkoani Njombe.
Mwishoni
mwa wiki jana Waziri mkuu alikuwa mkoani Njombe na kuzungumza na wakazi
wa maeneo mbalimbali ya halmashauri za wilaya Makete, Wangingombe, na
mji wa Makambako ambako ndio alianzia ziara yake.
Akiwa
Wangingombe alifungua jingo la Halimashauri ya Wangingombe na
kuzungumza na wananchi wa Mjia huo kasha kuwataka watumishi wa
halmashauri na wilaya kuhamia halmashauri hiyo ifikapo mwezi februari.
No comments :
Post a Comment