Monday, January 2, 2017

WATENDAJI WA SRIKALI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UFANISI


p-1
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk Khatibu akiwa katika moja ya majukumu yake walayani Chakechake.
……………………………………………………………………………………..
Na Masanja Mabula -Pemba ..
 
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk Khatibu amewataka watendaji wa Serekali kubadilike katika utendaji wao wa kazi ili waweza  kufanya kazi  kwa ufanisi zaidi na kila mmoja atekeleze majukumu yake ipasavyo  ya kazi na  kuacha  tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

Kauli hiyo ameitowa wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa serekali mara  baada ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kusherehekea miaka 53 ya mapindunzi  ya Zanzibar huko katika uwanja wa tensi chake chake.

Amesema kuwa lengo la kufanya usafi ni kuweka mazingira bora  katika Maosini hivyo ni vyema  wafanyakazi wanapohitajika kuonesha  ushirikiano wao katika kutekeleza majukumu hayo.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka watendaji wa Serekali kuelewa kwamba mapindunzi ya mwaka 1964 ndio yaliyofanikisha  uwepo wa wananchi kutokana na hekma za wazee waliokwisha tangulia hivyo ni vyema kuyathamini  na kuyaenzi matunda hayo ya Mapindunzi  na kuendelea kudumisha   amani na utulivu ndani ya nchi  .

Kwa upande wake Afisa Mdhamini ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais  Ali Salum Matta amesema kuwa sherehe za Mapindunzi zinalenga zaidi uzinduzi  wa  miradi mbali mbali ya maendeleo hivyo Serekali imejipanga kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo kwa nia ya  kuwaletea maendeleo  wananchi wake .

Aidha amewataka watendaji wa Serekali kushiriki kikamilifu katika sherehe hizo za uzindunzi wa miradi mbalimbali ya kijamii ambayo itafunguliwa , kukaguliwa na kuwekewa mawe ya msingi wakati wa sherehe hizo .

No comments :

Post a Comment