Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam
Umoja wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM) umesifu msimamo imara ulioonyeshwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujali na kupigania maslahi ya
wananchi wanyonge hatimaye kuzuia mpango batili wa Tanesco kupandisha
bei ya umeme nchini .
Pia Umoja huo umeelezea
kufurahishwa kwao na kuunga mkono uamuzi huo ambao umethibitisha kuwa
Dk Magufuli ni mtawala anayejali, kuthamini na kupigania maslahi ya
wananchi wanyonge na wenye vipato vya chini.
Matamshi hayo yametakwa
jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka mara baada ya kikao
cha watumishi wa UVCCM kutathmini utendaji wa mwaka 2016 na kuweka
mikakati ya utendaji kwa mwaka 2017 kilichofanyika katika ukumbi wa
UVCCM makao makuu Upanga Dar Es Saalam.
Shaka alikitaja kitendo
cha Rais Dk Magufuli kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco ) ameonyesha ujasiri, uzalendo na upendo kwa
wananchi ambao walimpa dhamana ya kuongoza dola .
Alisema haiwezekani Bodi
au Menijmenti ya Tanesco ifikie hatua ya kuamua au kupitisha maamuzi
mazito ya kitaifa na kupandisha bei ya umeme bila ya Waziri dhamana wa
Wizara ya Serikali asijulishwe .
“Tuko pamona na Dk
Magufuli , tunampa mkono wa heko kuzuia kupanda bei ya umeme ,
ametazama maslahi mapana ya wanabchi , hali za watu wanyonge na wenye
vipato vya chini, ametetea maslahi ya waliomuweka madarakani”Alieleza
Shaka.
Aidha alisema Tanesco
kwa kupitia Mkurugenzi wake na Waziri mwenye dhamana waliwaahidi
wananchi kwamba bei ya umeme katu haitapenada hivyo bei kama ingependa
na serikali kukaa kimya ingalikuwa ni kituko cha mwaka.
Kaimu katibu mkuu Shaka
aliwataka watendaji wa serikali , wakurugenzi wakuu wa mikoa, wajumbe wa
bodi makamishna, makatibu wakuu na wakurugenzi wa halamshauri za
wilaya waendelee kutekekeza majukumu yao kwa mujibu wa mipaka yao,
taratibu na shera bila kukurupuka.
“Watumishi na watendaji
wenye dhamana wakae wakijua mambo yamebadilika, zama hii si zama zile
zilizopita, Dk Magufuli na serikali yake ni makini huku wakifuatilia
kila pembe, atakayevimbisha mashavu ya ukaidi si ajabu akatubuliwa”
Alisisitiza Shaka
Hata hivyo UVCCM
imewahimiza watendaji na watumishi wa serikali waliopa katika sekta za
maendeleo kusoma upepo, kutenda haki na kutimiza wajibu na kwamba
maamuzi wanayopanga kuyapitisha ni lazima kwanza yajali maslahi ya
Taifa.
Shaka alifafanua kuwa
ni vyema ikafahamika na kueleweka kwamba Serilkali ya Chama cha
Mapinduzi imebeba imani, mioyo, matumaini na maisha ya watu hivyo umma
wakati unapokitegemea CCM , anapotokea mtu mmoja akaamua kuvuruga
utaratibu heri mtu huyo akawekwa pembeni.
“Tunaipongeza Serikali
ya CCM kwa kuendelea kusimamia nidhamu ya kazi, kupigania dhana ya
utumishi wa umma , uwajibikaji , uwazi pia kukomesha vitendo vya rushwa,
maonevu na ufisadi , tunamshauri Dk Magufuli aendelee kusimamia
majukumu yake bila kutikisika “Alisema Shaka
Alimaliza kwa kuusema
huku akiwataka watendaji dhamana kujipanga kimkakati na kimipango kwa
lengo la kutimiza ahadi zote zilizoanishwa katika ilani ya uchaguzi
ya CCM mwaka 2015 /2020 kwa sababu huo ndiyo mkataba kati ya wapiga kura
na Serikali ya CCM.
No comments :
Post a Comment