Binagi Media Group
Umoja wa waendesha bodaboda mkoani Mwanza umepongeza zoezi la ukaguzi wa vyombo hivyo linaloendeshwa na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.
Umoja wa waendesha bodaboda mkoani Mwanza umepongeza zoezi la ukaguzi wa vyombo hivyo linaloendeshwa na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.
Jana
Mwenyekiti cha umoja huo, Makoye Kayanda, amesema zoezi hilo
linaangazia maeneo makuu manne ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa
watumiaji wa bodaboda wakiwemo abiria.
“Cha
kwanza ni uvaaji wa kofia ngumu, cha pili leseni ya udereva, cha tatu
kuwa na BIMA na ni ubebaji wa mishikaki. Kuna baadhi ya abiria zaidi ya
14 wametozwa faini kwa kukataa kuvaa kofia ngumu, sasa lazima tufuate
sheria bila shuruti”. Alisema Kayanda huku akipongeza zoezi hilo.
Kayanda
aliwasihi waendesha bodaboda wote kuzingatia utii wa sheria bila
shuruti ili kuondokana na mazoea yanayoweza kuhatarisha maisha yao na
abiria wao pia huku akiwaonya baadhi ya abiria kuepuka tabia ya kukataa kutumia kofia ngumu kwa kisingizio cha uchafu.
“Kupanga
ni kuchagua, kama hutaki kuvaa kofia nguvu ya unayopewa na bodaboda,
nunua ya kwako ama mfuko wa plastiki ili ukipewa kofia uvalie maana kuna
watu wanapata ajali wanapasuka vichwa na inakuwa ni tatizo kwa familia
zao na taifa kwa ujumla”. Alihimiza Kayanda.
Mwenyekiti wa bodaboda mkoani Mwanza, Makoye Kayanda
No comments :
Post a Comment