Afisa Mawasiliano wa TBL Group Amanda Walter (Kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Meneja mkuu wa kituo cha televisheni cha TV 1,Joseph Sayi , wakati wa hafla ya tuzo kwa makampuni na taasisi zilizofanya vizuri katika nyanja mbalimbali ya Tanzania Leadership Awards 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Balozi wa Moroco nchini, Abdelilah Bennjane, (kushoto) akimkabidhi Meneja wa Chapa ya Ndovu ,Nicholous John (kulia) tuzo ya ushindi wa jumla kwa kipengele cha Mitandao ya kijamii ( Social Media Campaign of the year) TBL ilishinda kipengele hicho kupitia kampeni yake ya Mwagika Challenge Tanzania.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, Mohammed Mpinga, (kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa Mawasiliano wa TBL Group, Amanda Walter (katikati) na Meneja wa Chapa ya Ndovu ,Nicholous John wakati wa hafla ya Tanzania Leadership Awards iliyofanyika jijini mwishoni mwa wiki.Jeshi la polisi lilitunukiwa tuzo ya ubunifu wa huduma mbalimbali katika utendaji wake wa kazi -Most Innovative Service of the Year 2016
Afisa Mawasiliano wa TBL Group Amanda Walter na Meneja wa Chapa ya Ndovu ,Nicholous John wakiwa na tuzo ambazo TBL imejishindia
……………………………………………………..
Kampuni
ya TBL Group mwishoni mwa wiki iliendelea na rekodi yake ya kufanya
vizuri katika Nyanja mbalimbali ambapo ilifanikiwa kuzoa tuzo kuhusiana
na masoko na matangazo katika hafla ya Tanzania Leadership Awards iliyofanyika jijini mwishoni mwa wiki.
TBL
iliwepata tuzo kupitia chapa ya Ndovu Special Malt ambayo ilipata tuzo
ya jumla katika kipengele cha Print Ad of the Year na tuzo ya jumla
katika kipengele cha matangazo kupitia mitandao ya kijamii kupitia kampeni yake ya Mwagika Challenge Tanzania.
Akiongelea
ushindi huo,Afisa Mawasiliano wa TBL,Amanda Walter ,alisema kuwa
kampuni inajivunia ushindi huo wa tuzo hizo “Tuzo hizi zinadhihirisha
kuwa kampuni yetu inafanya vizuri katika nyanja mbalimbali ambapo
taasisi mbalimbali zinaona ubora wa kazi zetu na kutupatia tuzo ,kwetu
tuzo hizi zinazidi kutufanya wabunifu zaidi na tutaendelea kuboresha
huduma zetu na kushirkiana na serikali na taasisi zizizo za kiserikali
kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuleta maendeleo kwa nchi
yetu”.Alisema.
No comments :
Post a Comment