Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya , Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Emmanuel G. Lukula
…………………………………………………………………………..
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya
limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo
mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana
na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na
uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na
kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Mafanikio yaliyopatikana katika
msako ni kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya
saa 23:45hrs katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya
Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. EFRAHIM S/O
MWAITENDA, [60], mkazi wa Ntembela mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini,
alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu/watu wasiofahamika akiwa
amelala kitandani nyumbani kwake, mbinu ni kukata wavu wa dirisha na
kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za gololi,
nia ni kutaka kuumua. Mhanga amefikishwa Hospitali ya Rufaa na hali yake
inaendelea vizuri. Juhudi za kuwatafuta na kuwakamata zinaendelea.
Aidha mnamo tarehe 29.01.2017
majira ya saa 10:30hrs, katika mpaka wa nchi ya Mlawi na Tanzania
Kasumulu Wilayani Kyela, mfanyabiashara ajulikanae kwa jina moja la
JAPHET amekamatwa na kikosi maalumu [Task Force ] ya TRA , POLISI na
MAAFISA WAKILIMO akiwa anavusha mahidi kwa njia ya panya kutoka nchi
jirani ya Malawi bila ya kufuata utaratibu wa sheria za uingizaji
chakula nchini. Mahidi hayo yamekamatwa yakiwa kwenye gari moja aina ya
canter na mengine yalikuwa yamehifadhiwa kwenye store. Wakati wa
uchukuaji wa mahidi store kundi la wananchi walijitokeza na walianza
kuwazuia maafisa wa TRA kupakia mahindi hayo kwa kile walichodai kuwa
wanauziwa mahindi hayo kwa bei rahisi. Kutokana na hali hiyo Polisi
walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao.
Hata hivyo hali baada ya muda ilirejea kuwa shwari. Ufuatiliaji wa
karibu unaendelea ili kubaini wafanyabiashara wenye tabia kama hiyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G. LUKULA anatoa wito kwa
jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha
sheria pia anatoa onyo kwa wafanyabiashara wasiofuata sheria, kanuni na
taratibu za kusafirisha bidhaa iwe kutoa au kuingiza kwani mkono wa
sheria utawafikia kwani Jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau
wengine linaendelea kufanya misako ili kukomesha tabia hiyo. Aidha
anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu
kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi ya
wahusika.
[EMANUEL G. LUKULA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments :
Post a Comment