Naibu
Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson, akipeperusha bendera ya Taifa wakati wa
mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar
es Salaam jana. Dk.Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli kwenye
mkesha huo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Naibu
Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson (katikati), Mratibu wa mkesha huo Askofu
Godfrey Malesi na Askofu Damas Kenasi (kulia), wakishiriki kuomba
katika mkesha huo.
Waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifu mungu.
Watoto waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakifanya vitu vyao kwenye mkesha huo.
Waumini wakiwa wameinua mikono kwenye mkesha huo.
Maombi yakiendelea.
Wananchi wakisubiri kuupokea mwaka mpya wa 2017 katika uwanja huo.
Shamrashamra za kuupokea mwaka mpya.
Mwaka mpya wa 2017 ukipokelewa.
Wananchi wakiwa wamelala wakisubiri kuupokea mwaka mpya.
Na Dotto Mwaibale
NAIBU
Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson amesema Tanzania mpya na yenye matokeo
chanya kwa mwaka 2017 inawezekana hivyo akamataka kila mmoja wetu
kufanyakazi kwa bidii ili kuliletea taifa maendeleo.
Dk.Akson
aliyasema hayo kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli wakati akihutubia
kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam jana.
“Tanzania mpya na nchi mpya yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana” alisema Akson
Akson
alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli alikuwa mgeni rasmi kwenye mkesha
huo mkubwa ulioandaliwa na makanisa mbalimbali ya kiroho.
Akinukuu
baadhi ya maneno kutoka katika kitabu cha biblia cha Nyakati mungu
ataiponya nchi iwapo kila mtu atamuita kwa jina lake na kujinyenyekesha
na kuomba na kuziacha njia mbaya.
“Tukimuita mungu kwa jina lake na kujinyenyekesha kwa kuacha kutenda mambo mabaya mungu ataiponya nchi yetu” alisema Akson.
Mratibi
wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi alisema hivi sasa kila Januari Mosi
mikoa 17 hapa nchini imekuwa ikifanya mkesha huo ikiwepo na Zanzibar kwa
ajili ya kuwaombea viongozi wa nchi na taifa kwa ujumla.
“Mungu
amekuwa akijibu maombi yetu tangu tuanze kuomba kupitia mkesha huu
tulipoanza jijini Dar es Salaam mwaka 1997” alisema Malesi.
Alisema
tangu wakati huo wamekuwa wakiiombea nchi iwe na amani na kuondokana na
ufisadi na kumpata Rais atakayeifanya Tanzania iwe mpya ambapo
amepatikana Rais Dk.John Magufuli ambaye ameifanya nchi kuwa na muelekeo
mpya.
Alisema lengo lao ni kuhakikisha mkesha huo unafanyika katika mikoa yote na kila eneo la nchi yetu.
Mkesha
huo uliopambwa na nyimbo kutoka kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es
Salaam na Brass Band ya Polisi ulihudhuriwa na viongozi wa dini kutoka
nchi za jirani za Rwanda na Burundi ambao walipata fursa ya kuzungumzia
umuhimu wa nchi kuwa na amani.
No comments :
Post a Comment