Mkuu
wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu akipanda mti kuashiria uzinduzi rasmi
wa kampeni ya upandaji miti milioni moja na laki sita itakayopandwa
katika maeneneo mbalimbali wilayani kahama kwa lengo la kutunza
mazingira pamoja na kuufanya mji wa Kahama upendeze.
Mkuu wa wilaya kahama Fadhili Nkurlu akimwagia maji mti alioupanda wakati alipozindua kampeni ya upandaji miti
Mkuu wa polisi wilaya ya Kahama Mussa Mchenya akishiriki pia upandaji miti.
Afisa Usalama wa Wilaya ya
Kahama Aretus Lyimo akishiriki upandaji miti wakati wa zoezi la
uzindunzi wa upandaji miti milioni moja na laki sita.
Katibu Tawala wa Wilaya Kahama Timothy Ndanya akishiriki pia kupanda miti.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akifurahia wakati alipokuwa akipanda mti katika eneo la mgodi wa Buzwagi.
Meneja raslimali watu wa Mgodi
wa Buzwagi Solomon Rwangabwoba akifurahia kupanda mti wakati wa
uzindunzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja na laki sita
itakayoendeshwa na mgodi wa Buzwagi.
******************************************************
Afisa Mkuu Mwendeshaji wa
Kampuni ya Acacia Mark Marcombe akishiriki zoezi la upandaji miti
milioni moja na laki sita miti ambayo inatajwa kuwa itasaidia katika
kuipendezesha wilaya ya Kahama.
Afisa Mkuu wa Idara ya Raslimali watu wa Kampuni ya Acacia Peter Gereta akishiriki zoezi la upandaji miti.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya
Acacia anaeshughulikia Masuala ya Kampuni (Corporate Affairs) Deo
Mwanyika akishiriki pia kupata mti.
Mh. Salome Makamba MB-(Viti
Maalumu) akishiriki pia upandaji miti baada ya kupita karibu na eneo
ambapo zoezi la upandaji miti lilikuwa likifanyika na akaona ni vyema na
yeye akashiri katika kuunga mkono jitihada za Mgodi wa Buzwagi katika
kupanda miti itakayosaidia katika utunzaji wa mazingira wa wilaya ya
Kahama na Taifa kwa ujumla.
Afisa Mkuu wa Idara ya Utafiti
wa madini (Exploration) Peter Spora akifurahia wakati alipokuwa akipanda
mti katika eneo la Mgodi wa Buzwagi.
Taarifa kwa vyombo vya Habari:
Wakia Moja Mti Mmoja – Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi wajipanga kupanda miti milioni 1.6
Kahama: 31/01/2017. Mgodi
wa Dhahabu wa Buzwagi leo umezindua kampeni ya upandaji miti katika
Wilaya ya Kahama ikiwa na lengo la kupanda mti kwa kila wakia ya dhahabu
ambayo imechimbwa kwenye mgodi wa Buzwagi, ambapo miti zaidi ya milioni
moja na laki sita inatarajiwa kupandwa katika kipindi cha miaka miwili.
Akizindua
kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ameupongeza
uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa hatua hiyo na kusema ni ya kizalendo kwa
kuwa itasaidia katika kuboresha hali ya mazingira ya wilaya ya Kahama.
“Jukumu
la upandaji miti na kuhakikisha mazingira yetu yanatunzwa ni letu sote,
Wenzetu wa Buzwagi wameanza kuonyesha jitihada kwa kupanda miti milioni
moja na laki sita, hivyo sote kama Jamii hatuna budi kuwaunga mkono kwa
kuhakikisha kila mmoja wetu katika eneo lake anapanda miti na kuifanya
wilaya yetu ya Kahama izidi kupendeza”Alisema Nkurlu.
Akizungumzia
Malengo ya Kampeni hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo
amesema kama wadau muhimu wa mazingira wanalojukumu la moja kwa moja
kuhakikisha shughuli za utunzaji wa mazingira zinakuwa ni sehemu ya
maisha ya kila siku.
Na
kupitia mipango ya muda mrefu uongozi umejiwekea lengo la kupanda mti
mmoja kwa kila wakia moja ya dhahabu itakayokuwa ikizalishwa katika
kipindi chote cha uhai wa Mgodi wa Buzwagi ambapo inakisiwa mpaka
shughuli za uzalishaji zitakapositishwa takribani wakia milioni moja na
laki sita zitakuwa zimezalishwa.
“Leo
tunazindua awamu ya kwanza ya kampeni hii ambayo itahusisha upandaji wa
miti laki tano, ambapo mpaka sasa miti elfu ishirini imekwisha pandwa
na tunatarajia mpaka mwisho wa mwaka huu awamu ya kwanza ya miti laki
tano itakuwa imepandwa” Alisema Mwaipopo. “
“Kwa
kupanda miti hii, tunakusudia kuwa sehemu muhimu ya wadau wa mazingira
wenye lengo la kuipendezesha wilaya yetu ya Kahama, pia kukabiliana na
athari za mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuonyesha utayari wetu
kama Kampuni katika kurejesha katika hali ya awali ya mazingira ya eneo
la Mgodi itakapofikia wakati wa kuufunga. Aliongeza Mwaipopo.
Miti
aina mbalimbali inatarajiwa kupandwa katika zoezi hili huku mti maarufu
wa “Acacia” unaobeba jina la Kampuni mama ya Acacia Mining Plc
inayomiliki Mgodi wa Buzwagi ikiwa ni sehemu ya miti itakayopandwa,
Huku
zaidi ya shilingi milioni mia sita na arobaini na tano zikitarajiwa
kutumika katika awamu ya kwanza ya upandaji miti laki tano.
Katika
hatua nyingine maafisa wakuu wa Kampuni ya Acacia kutoka ofisi za
Acacia Mining Plc London pamoja na Dar es salaam walishiriki pia katika
zoezi la upandaji miti katika eneo la Mgodi wa Buzwagi wakati
walipofanya ziara ya kikazi mgodini hapo.
“Wakia Moja Mti Mmoja”
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano Mgodi wa Buzwagi
Simu +255 22 2164 200
No comments :
Post a Comment