Wednesday, January 4, 2017

MAMIA WAMUAGA RUBANI NA MTENDAJI MSTAAFU WA WAKALA WA NDEGE ZA SERIKALI MAREHEMU KENAN MHAIKI



Mama Mary Kenan (kulia), ambaye ni mjane wa marehemu akifarijiwa na dadake, Kenan Mhaiki Rubani Mtendaji mstaafu wa wakala wa ndege za serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam Januari 2 2017. Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda Songea Mjini Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4, Makaburi ya Matogoro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Leonard Chamriho akitoa salamu kwa niaba ya serikali wakati wa ibada ya misa na shughuli ya kumuaga Rubani na Mtendaji mkuu wa wakala wa ndege za serikali (TGFA) marehemu Kenan Paul Mhaiki shughuli iliyofanyika nyumbani kwake Kunduchi Dar es Salaam Januari 2 2017.Mwili wa marehemu umesafirishwa jana na kwenda Songea mjini Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika leo Januari 4 2017 kwenye makaburi ya Matogoro. 

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiaga mwili wa marehemu Kenan Mhaiki Rubani Mtendaji mstaafu wa wakala wa ndege za serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam Januari 2 2017. Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda Songea Mjini Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4, Makaburi ya Matogoro. (IMEANDALIWA NA ROBERT OKANDA BLOGSPOT)

Watoto wa marehemu Kenan Paul Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa baba yao wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam Januari 2 2017. Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda Songea Mjini Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika makaburi ya Matogoro mkoani humo Januari 4 2017.

Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani, Balozi Ombeni Sefue akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kenani Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam jana. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kwenda Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4 2017







Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Raymond Musingi akitoa salamu za pole kwa wafiwa.


Mkurugenzi Mkuu wa Usafiri wa Anga (TCAA) Hanza Johari  akitoa salamu za pole kwa wafiwa.




Waombolezaji wakimpa mkono wa pole Kaka mkubwa wa Kenan,Bw. Oliver Mhaiki, (kushoto)



Kaka wa Marehemu Oliver Peter Mhaiki akisoma wosia wa mwisho wa mdogoye Kenan.























No comments :

Post a Comment