Tuesday, January 31, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA CUF PROFESA LIPUMBA


 Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto), ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar
es Salaam.

 Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar
es Salaam.

 Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto) mara
baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

                                                 ………………………………………………………
Serikali ya Ufaransa kupitia Benki ya Maendeleo ya Nchi hiyo (AFD)
imeahidi kuwa inampango wa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kutoka wastani
wa euro milioni 50 hadi euro milioni 100 kwa mwaka katika miaka ijayo kwa ajili
ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Balozi wa
Ufaransa hapa Nchini Malika Berak ametoa kauli hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam
alipokutana na Kufanya mazunguzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu hatua zilizofikiwa katika uandaaji wa
kongamano la uwekezaji litakalofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia mwanzoni
mwa mwezi Aprili mwaka huu.
Balozi huyo
amesema mkopo huo itaiweza na kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali
ya maendeleo ya wananchi hasa katika sekta za maji na usafi wa mazingira na
miradi ya umeme.
Kuhusu uandaaji wa kongamano la
uwekezaji nchini
,
Balozi Malika Berak amemweleza Makamu wa Rais kuwa maandalizi ya kongamano hilo
kubwa la Kibiashara linalolenga kujenga na Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara
kati ya Tanzania na Ufaransa yanakwenda vizuri.
Balozi huyo
amesema kuwa kongamano hilo ambalo litakuwa la Kikanda litajadili kwa kina
fursa za uwekezaji hapa nchini hasa kwenye maeneo ya nishati, usafirishaji, teknolojia
ya habari na Mawasiliano na miradi ya maendeleo.
Balozi Malika
Berak amemhakikishia Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kuwa kongamano hilo
la kibiashara litawakutanisha pamoja wafanyabiashara  Watanzania na wenzao wa Ufaransa katika
kujadili na kubadilisha uzoefu katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kibiashara
kama hatua ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza Serikali ya Ufaransa
kupitia kwa balozi wake hapa nchi kwa ufadhili wa miradi mbalimbali ya
maendeleo hasa katika sekta ya maji na usafi wa mazingira, nishati na mapambano
dhidi ya umaskini nchini.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi wa Ufaransa hapa nchini
Malika Berat kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano yaliyopo
kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande Mbili yaani Tanzania na Ufaransa.
Makamu wa
Rais pia amepongeza jitihada za Serikali kupitia Ubalozi wake hapa nchini za
kuona umuhimu wa kuandaa Kongamano la kibiashara hapa nchini ambalo litatoa
fursa kubwa kwa watalaamu wa sekta mbalimbali nchini kukutana na kujadiliana
mambo kadhaa ikiwemo fursa za uwekezaji nchini.
 Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakt John Magufuli inaendelea
kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa kupambana na vitendo vya rushwa
kama hatua ya kuhamasisha wawekezaji wengi kuja kuwekeza hapa nchini.
Makamu wa
Rais amemweleza Balozi wa Ufarana hapa nchini kuwa milango ya ofisi yake ipo
wazi muda wote hivyo kama watakwama sehemu yeyote katika kuandaa kongamano hilo
amfahamishe haraka ili aweze kuchukua hatua haraka kusaidia mchakato huo
kutokana na muhimu wa kongamano hilo hasa wakati huu ambapo Tanzania inataka
kujenga uchumi wa viwanda nchini.

 Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba alipomtembelea ofisini kwake,
Ikulu Jijini Dar es Salaam leo

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba mara baada
ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

No comments :

Post a Comment