Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa
mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu. (PICHA NA IKULU)
|
NA
DAUDI MANONGI - MAELEZO.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wakuu
wa Mikoa,Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuondoa utitiri wa kodi uliopo
kwenye Mazao ili wakulima waweze kunufaika kutokana na kujiongezea kipato.
Agizo
hilo alimetolewa leo wakati akihutubia wakazi wa Wilaya ya Bukoba na watanzania
kwa ujumla akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera.
“Nawaagiza
Wakuu wa Mikoa,Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia upya Kodi
zilizopo katika bidhaa mbalimbali kama Kahawa na Pamba, hakikisheni mnaondoa
utitiri huu wa Kodi ili wafanyabiashara hawa wafaidike na mazao yao,” Alisema
Rais Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli amewaahidi watanzania kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na
mchana bila kujali itikadi, dini na makabila ili kuhakikisha nchi inasonga
mbele katika nyanja zote za kimaendeleo.
Akizungumzia
maendeleo ya michango mbalimbali kwa ajili ya wathirika wa tetemeko la Ardhi
mkoani Kagera Rais Magufuli amesema kuwa mpaka sasa simenti iliyochangwa ni
zaidi ya tani 30,600 na mabati zaidi ya elfu 31,000 ambapo wananchi wameshaanza
kupewa na kujengea.
Amewahimiza
wananchi walioathirika na tetemeko la Ardhi kutotegemea Serikali kuwafanyia
kila kitu na badala yake waanze kujenga na watumie msimu huu wa mvua kulima ili
kujipatia chakula.
Pia
Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza wahisani waliochangia Maafa ya Kagera
na kuwataka kuendelea na moyo huo katika kulijenga Taifa letu.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa
Bukoba mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara baada ya kuwasili katika shule ya
Sekondari Ihungo mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha wageni
pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa mkutano katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa
maeneo ya Ihungo Sekondari Mkoani Kagera
hawapo pichani mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika
Shule ya Sekondari Ihungo.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Charles Masinde
mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga nyumba yake mwenyewe mara
baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli amemuahidi mwananchi huyo kuwa atampatia mabati
30 kwa ajili ya kuezekea nyumba yake.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na balozi wa
Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi katika
ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule hiyo
inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani humo.
Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa
ukaguzi.
Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa
ukaguzi.
No comments :
Post a Comment