Wednesday, December 7, 2016

Yaliyojiri katika hafla ya Wafanyakazi wanawake TBL Group ya kufunga mwaka


Wafanyakazi wanawake wa kampuni ya TBL Group kupitia jukwaa lao la TBL Women’s Forum wamefanya hafla ya kuaga mwaka kwa mtindo wa aina yake ambapo wametumia fursa hiyo kuelimishana masuala mbalimbali kwenye mazingira yanayowazunguka ikiwemo kubadilishana uzoefu wa kazi na Maisha.
 
Pia walipata fursa ya kuwasikiliza watoa mada mbalimbali kutoka nje ya kampuni ambao walikaribishwa ambao waliongelea masuala ya afya,utunzaji wa nywele,ikimwemo umuhimu wa bima.
haf1
Meneja Masoko Msaidizi wa Jubilee Insurance Elieth Kileo,  akitoa elimu ya bima wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ilala jijini Dar es Salaam
haf2
Mmoja  wa wafanyakazi wa TBL Group akipokea  kipaza sauti kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa masuala yaliyoongelewa na mmoja wa watoa mada.
haf3
Mtaalamu wa masuala ya  urembo kutoka Abeer Naturals,Abigail Ambweni akitoa mada ya utunzaji wa nywele
haf4
Mtaalamu wa masuala ya  urembo kutoka Abeer Naturals,Abigail Ambweni,akionyesha jinsi ya kutengeneza nywele ili kuonekana maridadi.
haf5
Wafanyakazi wakimsikiliza mtoa mada,Sadaka Gandi,kutoka Lifestyle  Consultant
haf6 haf7 haf8
Wafanyakazi wakifurahia matukio mbalimbali kwenye sherehe hiyo

No comments :

Post a Comment