Na Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imsisitiza kuwa haitasita kuwatimua watumishi watakaobainika kula feha za miradi ya maendeleo na kukwamisha isikamilike kwa kuwa dhamira ya serikali ni kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi katika kuboresha maisha yao.
SERIKALI imsisitiza kuwa haitasita kuwatimua watumishi watakaobainika kula feha za miradi ya maendeleo na kukwamisha isikamilike kwa kuwa dhamira ya serikali ni kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi katika kuboresha maisha yao.
Waziri mkuu ,Kassim Majaliwa, ameyasema hayo Desemba 2 jijini
Arusha, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sheikh
Amri Abeid, na kusisitiza kuwa serikali inaendelea kuwakumbusha
watumishi wa serikali majukumu yao ya kutoa huduma bila upendeleo kwa
wananchi wake na akawataka wananchi wasisite kutoa taarifa iwapo hawatapatiwa huduma stahiki kwa wakati.
Amewataka
watumishi wote wa serikali kuhakikisha Wanaisoma Ilani ya uchaguzi ya
ccm na kuitekeleza hata kama hawaipendi cccm lazima waitekeleze kwa
vitendo na si vinginevyo.
Waziri
mkuu ameagiza kuanzia keso Jumapili magari aina ya Noah, kufanya huduma
ya kusafirisha abiria kutoka maeneno mbalimbali ya nchi kwa kuwa magari
hayo yametengenezwa yana uwezo wa kubeba abiria na haelewi kwa nini
Sumatra ilikuwa ikiyazuia.
Kuhusu eneo la soko la Kilombero, ambalo lilitolewa bila kufuata taratibu na kumilikishwa kwa mtu binafsi amesema ardhi ni mali ya serikali na eneo hilo kuanzia leo Desemba 2 ni mali ya serikali mara
baada ya kushinda kesi na akaiagiza halmashauri ya jiji la Arusha,
ikamilishe mchakato wa tathimini na kulijenga kwa ajili ya wananchi
kufanyia biashara .
Kuhusu maji amesema serikali imetoa shilingi bilioni 476 kwa ajili ya upatikanaji wa maji Arusha na tayari shilingi bilioni 2.6 zimeshakabidhiwa mamlaka ya maji safi na taka AUWSA.
Amesema serikali inaendelea kujenga bara bara za lami nchini kote na tayari wakandarasi wa bara bara wameshalipwa madai yao .
Amemuagiza
meneja wa Tanesco mkoa wa Arusha, kuhakikisha umeme haukatika katika
mkoa huo kwa kuwa tayari serikali imeshatoa fedha za kuboresha mfumo wa
umeme .
Katika
hatua nyingine Wazirri mkuu amekabidhi pikipiki maarufu Boda boda 200
kwa vijana wa maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha wakiwemo walemavu kwa ajili ya kuzitumia kuwawezesha kiuchumi.
No comments :
Post a Comment