Na: Frank Shija – MAELEZO
WATANZANIA
watakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika
Kukuza Uchumi kwa kujiunga pamoja na kuanzisha Viwanda vidogo vidogo na
vya kati.
Rai
hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah
alipokuwa akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kuhusu
maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania.
Akizungumzia
kauli mbiu ya maadhimisho hayo amesema kuwa inasadifu kile ambacho
Serikali imedhamiria kukifanya matharani suala zima la kuifanya Tanzania
kuwa nchi ya viwanda kitu ambacho kimeanza kutekelezwa.
“Watanzania
wanapaswa kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kutekeleza uanzishwaji
wa Viwanda vidogo vidogo na vya kati kwani kufanya hivyo kutapunguza ama
kuondoa kabisa tatizo la ajira kwa vijana,” alisema Bi. Zainab.
Aliongeza
watanzania wanapaswa kushirikiana kwa pamoja katika kuijenga Tanzania
ya Viwanda ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ndani na kuongeza fursa
ya ajira kwani viwanda ni eneo linalotoa ajira nyingi kwa wakati mmoja.
Aidha
Mkuu huyo wa Wilaya amempongeza Rais Magufuli kwa hatua kadha
alizokwishachukua katika kuhakikisha anaweka mazingira rafiki kwa
wawekezaji katika sekta ya viwanda akitolea mfano wa hatua ya Kampuni ya
Bakhresa kupewa eneo la ekari elfu kumi kwa ajili ya kujenga kiwanda
cha kusindika matunda.
Desemba
9 kila mwaka Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania
Bara ambapo kwa mwaka huu kitaifa yatafanyika Dar es salaam na kauli ya
mwaka huu ni “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuhimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu.”
No comments :
Post a Comment