Monday, December 5, 2016

WAMILIKI WA MITANDAO YA KIJAMII (BLOGGERS), HAWATASAJILIWA CHINI YA SHERIA MPYA: SERIKALI


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass, (watatu kushoto), akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Mtandao wa wamiliki wa Blogu Tanzania, (TBN), kwenye ukumbi wa mikutano ulio katika jengo la Jubilee Towers la PSPF jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa TBN, Bi. Khadija Khalili, Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao huo, Bw. Joachim Mushi na Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni msemaji mkuu wa serikali, Dkt. Hassan Abass, (watatu kushoto), akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Mtandao wa wamiliki wa Blogu Tanzania, (TBN), na mafunzo kwa wana mtandao hao kwenye ukumbi wa jengo la Jubilee Towers la PSPF jijini Dar es Salaam, leo Desemba 5, 2016

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas, amewaondoa hofu wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii nchini kupitia Mtandao wa Bloggers Tanzania, TBN, kuwa hawahusiki na usajili katika sheria mpya ya huduma za vyombo vya habari.
Dkt. Abbas ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Tanzania Bloggers Network-TBN, kwenye ukumbi wa Belmonte ulioko jingo la PSPF, Jubilee Towers jijini Dar es Salaam leo Desemba 5, 2016.
“Napenda niliweke wazi swala hili la waandishi kusajiliwa chini ya sheria hii mpya, ukweli ni kwamba, waendesha mitandao ya kijamii hawatahusika na swala la kusajiliwa ili afanye kazi hiyo,” alsiema
Aidha Mkurugenzi huyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali aliwaeleza wanamtandao hao kuwa, Utoaji wa Press Card, (Vitambulisho vya uandishi habari), kwa sasa utazingatia matakwa ya sheria ya sasa ya Huduma za vyombo vya habari lakini akawaondoa hofu kuwa, kanuni zitaundwa ili kuangalia pengine pawepo na press card zitakazozingatia madaraja mbalimbali (Categories).
“Ninawashauri ndugu zangu, mnatakiwa mjenge hoja ni kwanini mpatiwe Press Card, lakini uzoefu unaonyesha zipo baadhi ya nchi Duniani zinatoa press card kwa bloggers, pengine na hapa kwetu chini ya kanuni tutakazozitengeneza, tunaweza kutoa press card kwa bloggers pia.” Alifafanua.
Mkutano huowa TBN umedhaminiwa na benki ya NMB, PSPF, NHIF, Serengeti Beverarge Limited na Coca Cola.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abass, amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF leo Desemba 5, 2016.
Dkt. Abbas ambaye ameteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo, alijaza fomu za kujiunga na Mfuko huo akisaidiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi ofosini kwake jingo la Jubilee Towers barabara ya Ohio jijini Dar es Salaam.


Mtoa mada Krant Mwantepele


Dkt. Abass, akifurahia jambo na mmiliki wa Michuzi Blog, Bw. Muhidin Issa Michuzi, "Ankal"




Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.
Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili (kulia), akizungumza katika mkutano huo kuhusu masuala mbalimbali ya benki hiyo ambayo ni moja ya mdhamini wa mkutano huo.
Mwanahabari na Blogger  Frederick Katulanda (kulia), akiuliza swali.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (kushoto), akiwaelekeza jambo mablogger
Mablogger wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Mablogger kazini

Blogger Baraka kutoka Bukoba akiuliza swali.
Mwezeshaji wa mkutano huo Maxsence  Mello akitoa mada.
Meza kuu. Kutoka kulia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Krant Mwantepele.Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi pamoja na Katibu wa muda wa TNB, Khadija Kalili
Blogger Mroki Mroki akiwa kazini wakati wa mkutano huo.
Mgeni rasmi akihutubia.
Mwendeshaji wa mtandao wa FullShangwe, John Bukuku akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NMB wakibadilishana mawazo. Kushoto ni Doris na Joyce Nsekela.
Blogger kutoka mkoani Arusha, Tumaniel Seria (kulia), akiuliza swali. Kusho ni William Malecela mmiliki wa mtandao wa Mwananchi na katikati ni mmiliki wa Blog ya Michuzi Issa Michuzi.

Mmiliki wa mtandao wa Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akichangia jambo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja.

No comments :

Post a Comment