Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (kulia),
akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi
(kushoto) wakati akielezea mafanikio na changamoto zinazokikabili chuo
hicho. Kushoto kwa Mkuu wa Chuo ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
Bw. Mohamed Mtonga, Msaidizi wa Mkuu wa Chuo Dkt. Samwel Werema,
Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi– Ukaguzi Mamlaka za Mitaa Bw. Mwanyika
Musa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (kulia),
akijibu hoja zilizotolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt.
Faraji Kasidi (kushoto) alipofika Ofisi Kuu ya Chuo hicho kabla ya
kufungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi kutoka mikoa ya Kanda ya
Kaskazini.
Wakaguzi
wa Ndani kutoka Serikali za Mtaa na Sekretarieti za Mikoa wakiwa kwenye
mafunzo ya ukaguzi, Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo ni Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika. Mafunzo haya
yanafanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, mkoani Arusha.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika
(aliyesimama) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa ndani
ambapo alisema mpaka sasa wakaguzi wa ndani 308 wamepata mafunzo hayo
na wakaguzi 32 wameshafanya mafunzo hayo kwa vitendo.
Wakaguzi
wa Ndani kutoka Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa katika picha
ya pamoja. Waliokaa ni Mgeni Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
na Mipango Bi. Doroth Mwanyika kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha
Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa
Kiufundi Bw. Amin Mcharo na kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa
Serikali Mohamed Mtonga na Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali –
Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa.
Mgeni
Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth
Mwanyika (katikati) wakibadilishana mawazo na Kaimu Mkuu wa Chuo cha
Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi (Kushoto) na kulia ni Mkaguzi wa
Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika akimsikiliza
Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa
Bw. Mwanyika Musa ambapo alisema mafunzo hayo ni muhimu kwani yamelenga
kuimarisha ukaguzi wa miradi mikubwa ili ujenzi wake ulingane na thamani
ya fedha iliyotumika.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi akumfafanulia jambo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika.
No comments :
Post a Comment