Saturday, December 31, 2016

UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA MARUZUKU BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM WATOA SARE ZA SHULE KWA WATOTO 200


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Jabiri Sanze (kulia), akimkabidhi sare za shule mtoto, Hamad Ali Dar es Salaamleo, ambaye ataanza darasa la kwanza mwezi huu. Serikali ya mtaa huo imetoa sare za shule, daftari na penseli kwa watoto 200 watakaoanza darasa la kwanza mwaka huu wa 2017. Katikati ni mama wa mtoto huyo, Farida Rashid.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein akikata Utepe ikiwa ni ishara ya  ufunguzi  wa Msikiti,   Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Desemba 30, 2016. Wanaoshuhudia ni, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman (kushoto). (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)

 Rais akifunua kitambaa kuzindua msikiti huo
 Rais, akipokelewa wakati akiwasili kwenye ufunguzi huo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed wakati alipowasili katika ufunguzi wa msikiti, Masjid Muhammad (S.A.W) huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja leo Desemba 30, 2016. Msikiti huo umejengwa chini ya usimamizi wa Bw,Yakoub Othman mwakilishi wa Kampuni ya Al-Buwardy Tanzania.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Bw.Samir Ayoub mmoja wa wanafamilia ya Yakoub Othman, msimamizi wa ujenzi wa msikiti huo.

Sheikh Otman Maalim alipokuwa akitoa mawaidha baada ya ufunguzi wa  Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W)
 Rais akihutubia waumini baada ya ufunguzi huo
 Waumini waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa msikiti huo
Ni wakati wa sala

Rais wa Russia, Vladimir Putin


MAREKANI imetoa masaa 72 kwa wanadiplomasia 35 wa Russia kuondoka nchini humo ikiwatuhumu kuingilia uchaguzio mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Novemba pita.
Hatua hiyo inakwenda sambamba na kufungwa kwa majengo mawili yanayotumiwa na Russia kwa masuala ya kijasusi
Rais wa Marekani Barack Obama, amesema, hatua hiyo dhidi ya wanadiplomasia hao inafuatia ukiukwaji wa majukumu yao, kwa kufanya shambulio la kimtandao, (cyber attack), dhidi ya chama cha Democrat na aliyekuwa mgombea wake wa kiti cha Rais, Bibi Hilary Clinton.
Hata hivyo Russia imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na tuhuma hizo na kuita tuhuma hizo hazina ushahidi.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, imetangaza wanadiplomasia 35 wa Russia kutoka mji mkuu Washington na ubalozi mdogo wa Russia mjini San Francisco kuwa watu hao na familia zao hawatambuliwi na kupewa saa 72 wawe wamefungasha virago na kuondoka nchini humo.
Kremlin imesema haitalipiza kisasi na haina mpango wa kuwafurusha wanadiplomasia 31 wa Marekani walio kwenye miji ya Moscow na

Saint Petersburg


No comments :

Post a Comment