Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) akizungumza na Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam
kuhusu Kaya zilizoondolewa kwenye Mpango wa kunusuru Kaya Masikini
(TASAF), Awamu ya Tatu kwa kukosa sifa. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu,
Ikulu, Bw. Peter Ilomo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.
Serikali imeondoa kaya 55, 692 katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Awamu ya tatu kutokana na sababu mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) amesema hayo leo jijini Dar es salaam.
“Sababu za kuondolewa kwa kaya
hizo ni kifo, kuhama kijiji/mtaa ambapo mpango haujaanza kutekelezwa,
kutojitokeza mara tatu mfulululizo kupokea ruzuku, mnufaika kuwa mjumbe
wa kamati mbalimbali za mpango, wastaafu, viongozi wa watumishi wa
Umma.” Waziri Kairuki alisema na kuongeza hilo lilibainika baada ya
uhakiki alioagiza kufanyika mwezi Februari, 2016.
Waziri Kairuki alisema katika
uhakiki huo kaya zilizokuwa na mwanakaya aliyefariki au wote kufariki
zilikuwa 13, 898, kaya zilizohama vijiji/mitaa ambapo mpango haujaanza
kutekelezwa 6,228. Aliongeza kaya ambazo hazikujitokeza mara tatu
mfululizo kupokea ruzuku zilikuwa 17,746, zilizothibitishwa kuwa sio
masikini zilikuwa 13,468 na kaya zilizogundulika kuwa na baadhi ya
wanakaya wajumbe wa kamati za usimamizi za Jamii, Halmashauri za
Vijiji/Kamati za Mitaa, Viongozi na watendaji zilikuwa 4,352.
Mhe. Kairuki aliainisha kuwa
kufuatia agizo lake alilotoa mwanzoni mwa mwaka huu hadi Septemba 2016
kiasi cha shilingi 6,427,110,309 kimeokolewa kwa kaya 42, 035
zilizoondolewa kwa kipindi hicho, na kusisitiza kiasi hicho kitaongezeka
kwasababu zoezi hilo linaendelea.
Waziri Kairuki alifafanua kuwa
ameshauriana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuwasimamisha
waratibu wa TASAF Wilaya na uchunguzi kufanyika wa jinsi
walivyojihusisha kuvuruga utekelezaji wa mpango kwa kuandikisha kaya
zisizo na sifa.
Kufuatia hilo, Waziri Kairuki
alimwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF kuwasimamisha kazi mara moja
na kuendelea na hatua za kinidhamu kwa Maafisa Washauri na Ufuatiliaji
106 walioko kwenye Halmashauri walioshindwa kufuatilia na kusimamia
mpango hivyo kusababisha kaya zisizostahili kuingizwa kwenye Mpango na
kuendelea kulipwa isivyostahili.
Wengine alioelekeza kusimamishwa
ni Maafisa watano wa TASAF Makao Makuu wanaosimamia mpango, pamoja na
Mameneja Uratibu na Mkurugenzi wa Uratibu ambao ndio wasimamizi wakuu.
Pamoja na hayo, Waziri Kairuki ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina
kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja ili kubaini ushiriki wa Maafisa hao
na kuchukua hatua stahiki kwa wale watakaothibitika kuhusika katika
kuvuruga utaratibu wa utekelezaji wa mpango au kuwepo udhaifu katika
usimamizi, ufuatiliaji na uwajibikaji.
Waziri Kairuki alielekeza Wakuu
wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, Majiji,
Manispaa, Miji na Wilaya wahakikishe kuwa fedha zote zilizotolewa kwa
kaya zisizokuwa na sifa zinarejeshwa ili ziwanufaishe walengwa.
Waziri Kairuki alitoa rai kwa
wananchi na wadau wote wa Mpango wa TASAF kutoa taarifa za watu wote
ambao wananufaika lakini hawastahili kuwa kwenye Mpango ili malipo
yasifanyike kwa wote wasiostahili.
Awamu ya Tatu ya TASAF ilianza
mwaka 2012 ambapo Serikali inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.
Kaya zilizoandikishwa idadi yake ni 1,110,635, na kaya hizo
huandikishwa baada ya hatua ya utambuzi ambayo jamii husika
hushirikishwa katika mikutano ya pamoja kwa kuweka vigezo vya umasikini
na baadaye kaya hizo hufanyiwa uhakiki kwa kutumia takwimu na viashiria
vya umasikini. Takwimu zinaonyesha kuwa Watanzania takribani 28.2% bado
ni masikini sana, na serikali hadi sasa imeshatumia shilingi
391,835,484,755 zilizolipwa katika mikupuo nane kwa kaya 1,110,635
No comments :
Post a Comment