Mameneja wa Vitengo cha Uhasibu wa TBL Group kutoka kushoto, Alois Qande na Edward Peter wakifurahia tuzo ya ushindi.
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Uhasibu na ukaguguzi wa mahesabu nchin (NBAA) Pius
Maneno akimpongeza mfanyakazi wa TBL Group Alois Qande mara baada ya
kuibuka mshindi wa Tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu wa mwaka 2015
wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine kwenye picha
wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Isaya Jairo na
Kamishna Shogholo Msangi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
Mhasibu Mwandamizi wa TBL Group, Alois Qande akipokea tuzo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Kamshna Shogholo Msangi.
Mhasibu Mwandamizi kutoka TBL Group akibadilishana mawazo na watendaji wa NBAA,Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA , Pius Maneno, Mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Isaya Jairo na Kamishna Shogholo Msangi.
Wafanyakazi wa TBL Group wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wengine kutoka makampuni mbalimbali.
……………………………………………………………………………………
Kampuni ya TBL Group imezidi kung’ara katika tuzo ya utunzaji wa mahesabu na uwasilishaji wa taarifa za fedha katika shindano linalotayarishwa
na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa mahesabu (NBAA) kila mwaka na
kuhusisha taasisi za serikali na makampuni binafsi katika sekta
mbalimbali.
Mwaka huu TBL Group imeshika nafasi ya pili katika sekta ya viwanda vikubwa ambapo mwaka jana iliongoza na kutunukiwa tuzo ya ushindi wa jumla wa shindano hilo.
Akiongea muda mfupi baada ya kutunikiwa tuzo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaamya uwakilishaji ,Mhasibu mwandamizi kutoka TBL Group, Alois Qande, alisema kuwa kampuni
hiyo itaendelea kuwa mfano wa uwekezaji wenye tija na itaendelea
kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuweka kipaumbele katika
kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi kwa wakati mwafaka.
“Tuzo kama hizi kwetu TBL Group tunazithamini sana kwa kuwa zinaleta
motisha kwetu na kufanya kampuni itambulike kitaifa na kimataifa na
natoa wito kwa watanzania wote kununua na kuzitumia bidhaa
zinazozalishwa na makampuni ya hapa nchini kwa kuwa ndizo zinasababisha nchi kukua kiuchumi na kuondokana na umaskini”.Alisema.
Amesema
kampuni imejipanga kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi wenye viwango ili
kukuza sekta ya viwanda nchini na kuongeza fursa za ajira kwa
watanzania “Kupitia biashara ya kampuni idadi kubwa ya watanzania
wanaendelea kunufaika kupitia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja
kwa moja”.Alisema.
No comments :
Post a Comment