Taasisi
ya MO Dewji Foundation imeweza kuwakumbuka watoto wanaopatiwa matibabu
ya magonjwa ya kansa katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo ndani
ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Katika
kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwemo kuingia mwaka mpya wa
2017, MO Dewji Foundation imeweza kutembelea watoto wa kituo hicho cha
Tumaini la Maisha na kutoa zawadi kwa watoto hao ili kuwasaidia katika
kipindi wawapo kituoni hapo wakiendelea na kliniki ya matibabu yao.
Kwa
zaidi ya miaka mitatu MO Dewji Foundation imekuwa ikitoa ufadhili na
mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto hao, mafunzo kwa watoto
hao wawapo kituoni hapo, gharama za usafiri kwa watoto kuja na kurejea
kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya matibabu yao katika wodi yao
iliyopo Hospitalini hapo Muhimbili. Katika tukio hilo, Mo Dewji
Foundation waliweza kutoa vitu mbalimbali kama zawadi kwa ajili ya
kusaidia mahitaji ya kituo hicho.
Miongoni
mwa vitu hivyo ni pamoja na unga wa ngano, sabuni za kunawia mikono,
sabuni za kuogea, doti za khanga, mafuta ya kupikia na vitu vingine
vingi. Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez
amewatakia kila lakheri watoto na wazazi wa kituo hicho katika kuingia
mwaka mpya ambapo pia aliwahakikishia wafanyakazi wa kituo hicho kuwa
taasisi yao itaendelea kusaidia kituo hicho.
Mkuu
wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akimkabidhi Mwalimu Leonard
ambaye ni mwalimu anayetoa elimu kwa watoto wenye kansa wanaopatikana
kituoni hapo.
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akikabidhi zawadi hiyo kwa mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho cha TLM
Mkuu
wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akiwa katika picha ya pamoja
na wafanyakazi wa kituo hicho, pamoja na baadhi ya watoto hao wa TLM.
Mratibu
wa Miradi wa MO DEWJI Foundation, Catherine Decker akiwa pamoja na
watoto wa TLM, wakati wa tukio hilo la kuwafariji watoto pamoja na kutoa
zawadi.
Mwalimu Leonard wa TLM akiwa na mmoja wa watoto wa kituo hicho wakati wa tukio hilo la kutoa zawadi.
Jengo la TLM
No comments :
Post a Comment