Na Jonas Kamaleki, Paris
Serikali inakumbwa na changamoto
kuu mbili katika kutekeleza Mpango wa Uendeshaji Serikali kwa Uwazi
(OGP) ambazo ni kutoa huduma kwa wananchi na kujitathimini yenyewe.
Hii ni kauli ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Twaweza, Bw. Aidan Eyakuze aliyoitoa jana jijini Paris,
Ufaransa wakati wa mjadala wa jopo la wataalam wa OGP baada ya ufunguzi
wa Mkutano wa Kilele.
“Kutatua changamoto ni pamoja na
kufanya kazi na wananchi na kuwasikiliza nini wanataka badala ya wewe
kuwaletea,” alisema Eyakuze.
Aliongeza kuwa lazima kuwepo
utoaji wa fursa ya wananchi kujaribu hata ikitokea wakashindwa kutimiza
malengo lakini wamepewa nafasi.
Eyakuze alisema katika utekelzaji
wa OGP yapo matunda mawili ambayo ni mazungumzo ya kudumu baina
Serikali na wananchi pia na mkakati wa kujitathimini. Bila mazungumzo na
kujitathini uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi hauwezi kutimia,
alisisitiza Eyakuze.
Aridudia maneno ya Rais wa
Ufaransa, Francois Hollande kuwa demokrasia ikishambuliwa haiwezi kurudi
nyuma lazima isonge mbele ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Kwa upande wake, Rais Hollande
alisema: “Tunataka demokrasia inayoaminika na ya kupambana na rushwa na
vitendo viovu katika jamii.”
Aliongeza kuwa ili kupunguza
vitendo vya rushwa na kuongeza uwazi katika Serikali, nchi yake imetunga
sheria ya kuwalinda watoa taarifa.
“Viongozi wa Serikali ikiwemo
wabunge na mawaziri ni lazima kutangaza mali zao kwa ajili ya kudhibiti
mianya ya kujilimbikizia mali wakiwa madarakani,” alisema Hollande.
Ili kufanikisha Mpango wa
Uendeshaji Serikali kwa Uwazi ni lazima wananchi kushirikiana na
Serikali yao, aliongeza Rais Hollande.
Huu ni Mkutano wa Kilele wa 4
ambao umejumuisha mataifa toka pande zote za Dunia ambao ni wanachama wa
OGP na wale ambao wanataka kujiunga na Mpango huo. Unafanyika jijini
Paris, Ufaransa kwa siku tatu.
Katika siku ya ufunguzi nchi
kadha zimejiunga na mango huo. Nchi hizo ni pamoja na Ujerumani,
BurkinaFaso, Jamaica, Luxembourg, Pakistan, Ureno na Senegal. Nchi
ambazo zinakaribia kujiunga ni Afghanistan, Madagascar na Morocco.
Suala kubwa katika Mkutano huu wa
Kilele ni Uwazi na kupambana na rushwa katika Serikali za nchi
wanachama. Uwazi unatakiwa katika kutengeneza bajeti za nchi, katika
kutoa kandarasi na utoaji wa wa taarifa kwa wananchi kwa uwazi zaidi.
No comments :
Post a Comment