Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wamiliki wa Bloggers
Tanzania kabla ya kufunga mafunzo kwa mablooger hao yaliyofanyika Jijini
Dar es Salaam.
Na Beatrice Lyimo-
MAELEZO Dar es Salaam.
SERIKALI inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na
semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la
tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti
ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa
heshima tasnia ya habari nchini.
Aidha, Waziri Nape alisema kuwa
tayari Serikali imeanza mazungumzo na makampuni na taasisi mbalimbali
kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi
wanapatikana kwa uwazi.
“Tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa
namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo makampuni zaidi
yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo yatakayojielekeza
kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.
Waziri Nape pia alisema amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.
“Tutumie fursa za kisiasa
zilizopo, fursa za teknolojia ili kuhakikisha tiunajenga Tanzania
tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa kutumia taaluma mliyonayo ili kuweza
kuipeleka nchi ya Tanzania tunayoitaka” alifafanua Waziri Nape.
No comments :
Post a Comment