Thursday, December 8, 2016

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, akiongoza kikao cha baraza LA mawaziri, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 7, 2016.(PICHA NA IKULU).


 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wahariri  kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari uliyopitishwa na Bunge pamoja na kujadili mpango mkakati wa TEF wa kuendeleza tasnia ya habari nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.


Mkuu wa Majeshi ya  Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (Wa pili kushoto) pamoja na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Salvatory Mabeyo (Wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na ma Meja Jenerali wapya, mara baada ya kuvishwa vyeovyao vipya Makao Makuu JWTZ Upanga Dar es Salaam.(PICHA NA JWTZ)


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange (kushoto) akimvisha cheo cha Meja Jenerali Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Michael Isamuhyo, Makao Makuu JWTZ Upanga Dar es Salaam.



Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, (JWTZ),  Jenerali Davis Mwamunyange (Kushoto), akimvisha cheo cha Meja Jenerali, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Brigedia Jenerali George William Ingram,Makao Makuu JWTZ Upanga Dar es Salaam.

No comments :

Post a Comment