Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Bw. Charles Mwijage akisikiliza maelekezo kuhusu usajili wa
wajasiriamali katika fao la hiari kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma( PSPF) Bw.Hadji Jamadar wakati wa
hafla ya ufunguzi wa maonesho ya kwanza ya Viwanda vya Tanzania katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan
Trade) Bw. Edwin Rutageruka.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Hadji Jamadar akielezea jambo
kwa wateja waliotembelea banda la mfuko huo katika maonesho ya Viwanda
yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
………….
Na Jacquiline Mrisho
Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umetoa rai kwa wajasiriamali...
kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari ili kuweza kupata huduma ya
hifadhi ya jamii.
Rai
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Uendeshaji wa mfuko
huo, Hadji Jamadary wakati wa uzinduzi wa maonesho ya kwanza ya viwanda
vya Tanzania uliofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini humo.
Jamadary
amesema kuwa mpango huo utawawezesha wananchi wasio na ajira rasmi
kupata fursa ya huduma ya hifadhi ya jamii kama wapatavyo wanachama
wenye ajira rasmi pia unawawezesha wanachama walio katika mfuko huo
kuweza kujiwekea akiba ya ziada.
“Mpango
huu wa hiari ni mfuko ulio huru ambao unamruhusu mwananchi yoyote
mwenye umri kuanzia miaka 18, mwenye uraia wowote hata kama anafanya
kazi ndani au nje ya nchi, hivyo tunawaomba wananchi wote kuchangamkia
fursa hii kwa manufaa ya maisha yao ya baadae,”alisema Jamadary.
Ameongeza
kuwa hadi sasa mfuko una jumla ya wananchi 98,733 ambao tayari
wamejiunga na mfuko huo lakini kwa kutambua umuhimu wa mfuko huo zaidi
ya wananchi 102 wameshajiunga wakati maonyesho hayo yanayotarajiwa
kumalizika mnamo Disemba 11 mwaka huu yakiendelea.
Aidha,
Afisa huyo ametaja jumla ya mafao 6 yaliyopo katika mfuko huo yakiwemo
ya elimu, ujasiriamali, uzee, kifo, ugonjwa au ulemavu, matibabu na fao
la kujitoa pia mfuko huo unatoa fursa kwa mwanachama kukopa nyumba na
viwanja.
Kuhusiana
na fao la matibabu, Jamadary amefafanua kuwa mwanachama atapatiwa bima
ya afya yenye gharama ya shilingi 76,800 kwa mwaka mzima pia
ataruhusiwa kuwaingiza wategemezi watano ambapo kila mmoja atalipiwa
kiasi hicho cha fedha kwa mwaka mmoja.
Mpango
wa hiari umeanzishwa mwaka 2013 ukiwa na lengo la kupanua wigo wa
uanachama kwa kuandikisha wananchi waliojiajiri au kuajiriwa katika
sekta rasmi au isiyo rasmi.
No comments :
Post a Comment