REA AWAMU YA TATU KUJA NA NGUZO ZA ZEGE
GAZETI LA NIPASHE YAFANIKISHA WANAFUNZI KUONDOKANA NA PAA LA NYASI.
WANANCHI wa kijiji cha Yitwimila A kilichopo kata ya Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu wamelipongeza gazeti la NIPASHE kwa kuandika ukweli wa mambo yanayojitokeza katika sehemu mbali mbali ikiwemo habari yao ya kuezekwa kwa nyasi shule ya msingi Masanza kuonekana na kuchukua sura ya pekee katika jamii na nchi kwa ujumla.
Pongezi hizo zimekuja siku chache tu mara baada ya gazeti hilo lilipotangaza juu ya shule ya Masanza kuezekwa kwa nyasi na wazazi wa eneo hilo ili kuweza kuwasaidia watoto waliokuwa wakisoma katika hali ngumu ya kupigwa na jua kwa muda mrefu.
Samwel Abel ni mkazi wa kijiji hicho anaeleza kuwa ni juhudi za wananchi zilizofanikisha kumtafuta mwandishi wa habari wa NIPASHE ili aweze kurusha habari ya shule hiyo na jinsi gani wanafunzi wanavyopata shida wakati wa masomo wanapokuwa juani.
“Si wanafunzi tu bali hata walimu ambao ndio wasimamizi wakuu wa maendeleo ya watoto pindi wanapokuwa shuleni lakini nao walikuwa wakikumbana adha kubwa kama hiyo ya kufundishia juani,hii ni aibu kubwa sana kwani jengo hilo lilimalizwa na wananchi kwa muda wa miaka zaidi ya 3 na kukaa tu huku wanafunzi wakisomea juani alisema”
Kwa upande wake Christina Joseph ni mkazi wa kitongoji cha nyawa anaeleza kuwa wanampongeza mbunge wa jimbo la Busega Dr Raphael Chegeni kwa kuweza kujitolea kwa kuezeka shule hiyo.
Bi Chrisitina aliongeza kuwa wanajipongeza wao kama wananchi kwa kufanya kitu ambacho kimewaletea maendeleo ya haraka katika shule yao,kwani bila kuiezeka shule hiyo kwa majani basi mpaka leo kusingekuwa na dalili za kuezekwa kwa shule hiyo.
Aidha tunalipongeza gazeti la NIPASHE kwa umakini wake wa kuandika habari za watu wa chini kama ilivyo sera ya Rais Magufuli ya kuwahudumia watanzania wa hali ya chini na hii imejionyesha kwa gazeti hilo kwani limetenda haki kwa jamii ya chini.
Na kwa upande wake mbunge huyo wa Busega Dr Raphael Chegeni alipopigiwa simu alisema kuwa suala la wananchi kuezeka nyasi shule ni kitendo cha ujasiri sana kwao ingawa ni aibu kwa serikali lakini tumelimaliza na sasa mabati yameshaezekwa shuleni hapo ili kuweza kuwasaidia wanafunzi hao.
Aliongeza kuwa pesa za mfuko wa jimbo atazipeleka zote katika kuhakikisha majengo yote yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi anaziezeka ili wanafunzi wapate mahali pa kusomea.
“Nimemuomba mkurugenzi aweze kunipatia idadi ya majengo yote ambayo bado ayajaezekwa ili pesa za jimbo zimalizie kero hiyo
No comments :
Post a Comment