Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.
Mpoki Ulisubisya (kushoto), akihutubia wakati akizindua Baraza la tatu
la Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wafanyakazi MSD, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean
Bwanakunu (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakielezwa na viongozi wao katika mkutano huo.
![]() |
| Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa kwenye mkutano huo. |
Na Dotto Mwaibale
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.
Mpoki Ulisubisya amewaasa watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) kuhakikisha
kuwa ...wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupunguza malalamiko ya
wananchi juu ya ukosefu wa dawa.
Katibu
Mkuu huyo ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akizindua Baraza la
tatu la Wafanyakazi la Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pia amesisitiza kuwa
Baraza hilo libuni mbinu na mikakati mbadala za kuboresha utendaji bila
kusahau kutii miiko ya utumishi wa umma.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wafanyakazi MSD, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean
Bwanakunu amemweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuwa tayari MSD
imeanza kununua dawa na vifaa tiba kutoka kwa wazalishaji, ambapo hadi
sasa wanawazalishaji 20 ambao wanamikataba, na wazabuni wengine 76
wadawana 79 wa vifaa tiba zabuni zao zinaandaliwa.
Mkutano
huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka Makao Makuu ya MSD na Kanda zote nane
za MSD ambao ni pamoja na Mwenyeviti wa Tughe na matawi pamoja
wawakilishi wa wafanyakazi.





No comments :
Post a Comment