Friday, December 30, 2016

michezo kwa Vijana kutangaza Utalii Nyasa


Manyanya
[Ruvuma] Mbunge wa Nyasa, Mh. Injinia Stella Manyanya amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusadia kutangaza utalii wa Wilaya ya Nyasa  kupitia vijana kupitia michezo ili kukuza Utalii na Utamaduni uliopo Wilayani humo.

Hayo ameyasema katika tamasha la kutangaza Utaliii wa Wilaya  ya Nyasa   ulioshirikisha uongozo wa Selikali kupitia mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na wadau wengine.
“Wadau mbalimbali tunao msingi wa kujitokeza na kutangaza Utalii wetu ndani ya Nyasa hasa kupitia Vijana wetu. Vijana ndio wenyewe wenye fursa wa kukuza utalii kupitia njia mbalimbali, ikiwemo Utalii wa Michezo, Elimu,Afya, Uvuvi, Kupanda Milima, kuvua usiku na utalii mbalimbali hivyo kupitia michezo hii italeta hamasa kubwa Nyasa” alieleza Mh. Injinia Stella Manyanya.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Nyasa, Bi.Isabela Chilumba amesema  Mikoa ya Kusini inanafasi ya kuutangaza Utalii  kupitia michezo mbalimbali ambayo pia inaweza kuiinua pato la  taifa licha ya kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa na viwanja vya michezo.
Aidha amebainisha kuwa, mikoa ya Kusini na mingine nchini bado aijaiitumia Michezo  kama njia ya kutangaza Utalii na utamadu wa  maeneo husika.
Nao baadhi ya wachezaji w a Team hizo  ambazo ni Yatima na Kilosa wameeleza michezo hiyo licha ya kutangaza utalii lakini kwao ni ajira na itasiaidia kuwapatia kipato kwani kuonesha uwezo wao itatoa fursa ya kujiendeleza kimichezo na kuinua vipato vyao,alieleza Raphael Saimon Mchezaji  wa timu ya Yatima-Nyasa.
Kwa upande wake Samson David  ambaye ni mchezaji wa timu ya Kilosa-Nyasa amesema kupitia michezo itawasaidia kuwaondoa vijana katika makundi mabaya ikiwemo ya vijiweni.

No comments :

Post a Comment