Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za
Jamii Epharaim Kwesigabo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu
hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba mwaka huu, kulia kwake ni
Mtakwimu Bw. Muhidini Mtindo.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za
Jamii Epharaim Kwesigabo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu
hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba mwaka huu, kulia kwake ni
Mtakwimu Bw. Muhidini Mtindo.
Wanahabari wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epharaim Kwesigabo (hayupo
pichani) wakati akielezea hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba mwaka
huu.
Picha na Benjamin Sawe-Maelezo.
…………………
Na.Alex Mathias na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi
Novemba 2016 umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.5
toka mwezi wa Octoba, 2016 kutokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa
na huduma mbalimbali za mahitaji katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo, amesema kuwa bidhaa
za vyakula zikiwemo ngano,mbogamboga, mtama,Mahindi pamoja na vinywaji
vya baridi zimechangia kuongezeka kwa mfumuko huo.
“Bidhaa nyingine zilizochangia
kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni Nishati , mafuta na viatu huku
akibainisha kuwa kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa
na huduma zinazotumiwa na kaya nchini zimeongeka na kufikia 104.32 kwa
mwezi Novemba 2016 ikilinganishwa na 99.54 za mwezi Novemba mwaka jana”
Alisema Kwesigabo.
Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi ameeleza kuwa umeongezeka kwa asilimia 1.1 kwa mwezi Novemba ikilinganishwa na asilimia 0.1 ya mwezi Octoba kutokana na kuongezeka kwa Fahirisi ya baadhi ya bidhaa zikiwemo unga wa ngano, unga wa mihogo, unga wa mahindi, mtama, dagaa, mchele.
Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi ameeleza kuwa umeongezeka kwa asilimia 1.1 kwa mwezi Novemba ikilinganishwa na asilimia 0.1 ya mwezi Octoba kutokana na kuongezeka kwa Fahirisi ya baadhi ya bidhaa zikiwemo unga wa ngano, unga wa mihogo, unga wa mahindi, mtama, dagaa, mchele.
Aidha, alisema kuwa thamani ya
shilingi ya Tanzania hupima badiliko katika kununua bidhaa na huduma
zilezile za mlaji ambazo shilingi ya Tanzania ingeweza kununua katika
kipindi tofauti, ikiwa fahirisi za bei za Taifa zinaongezeka uwezo wa
shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma hupungua.
Kwa upande wa mfumuko wa bei wa
Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki Kwesigabo alisema kuwa
una mwelekeo unaofanana ambapo Kenya umeongezeka na kufikia asilimia
6.68 mwezi Novemba kutoka 6.42 za mwezi Octoba huku Uganda ikiwa na
mfumuko wa bei wa asilimia 4.6 mwezi Novemba kutoka asilimia 4.5 za
mwezi Octoba
Anamalizia kwa kusema kuwa Sensa
hii ni ya mikoa yote nchini na sio Dar es salaam kwa kuwa huwa wanafanya
utafiti kwa kila mwezi ili kujua kama kuna ongezeko au punguzo la
bidhaa limetokea hivyo wamewataka waandishi kufikisha ujumbe kwa jamii
ili waweze kujua ongezeko ambalo limepanda toka mwezi Oktoba hadi sasa.
No comments :
Post a Comment