Mkurugenzi
wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida (katikati mwenye tuzo), akiwa na
wafanyakazi wenzake baada ya kutunukiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa
Mahesabu Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
Mgeni
rasmi katika hafla hiyo akisoma hutuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na
Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na katikati ni Mkurugenzi
Mkuu wa NBAA, Pius Maneno.
Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi
wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo.
Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi NBAA. Profesa Isaya Jairo.
Wapiga picha za habari wakiwa tayari kwa kazi.
Wafanyakazi wa Mfuko wa LAPF wakipita meza kuu baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MFUKO wa
Pensheni wa LAPF, umetunukiwa tuzo ya kuwa kinara katika utunzaji wa
mahesabu dhidi ya mifuko mingine ya hifadhi ya jamii nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu
wa mfuko huo, Elyudi Sanga baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa
Fedha wa mfuko huo, John Kida, alisema kwao ni mafanikio makubwa kwa
kupata tuzo hiyo.
“Tunatumia
njia za kisasa ya utunzaji wa mahesabu huku tukifunga mahesabu yetu kwa
wakati jambo linalotupa fursa ya kuweka sawa mambo yetu ya mahesabu”
alisema Kida.
Alisema wamekuwa wakifunga mahesabu yao kwa kiwango cha kimataifa ndio maana wamekuwa wakiibuka washindi mara nyingi.
Kida alisema kuwa ushindi huo ni wa mara ya nane tangu kuanzishwa kwa utoaji wa tuzo hizo mwaka 2008.
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe, alisema kuwa wanachama wao
wanatakiwa kuendelea kuwa na imani na mfuko wao na kuwa fedha zao zipo
kwenye mikono salama.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Pius
Maneno, alisema makampuni na taasisi 56 zilishiriki katika mashindano
hayo kwa mwaka huu ambapo waligawanywa katika makundi 12 kulingana na
huduma wanazozitoa.
Alisema
tuzo hizo zina lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji katika suala zima
la mahesabu na kuhakikisha viwanago vya kimataifa vinazingatiwa katika
utunzaji wa mahesabu.
Aliwataka
wahasibu nchini kuandaa taarifa bora za fedha ili kuboresha hesabu za
mashirika na makampuni na kuongeza uwazi katika shughuli zao.
Tuzo hizo
ziliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) na
zilitolewa juzi katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (ACP) kilichopo
Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment