Mbunge
wa Viti Maalum Kigoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Josephine
Gezabuke ametuhumiwa na viongozi wa chama hicho wilaya ya Kasulu
kushiriki kutaka kumn’goa Meya wa Halmashauri ya Kasulu, Twaribu Mangu
licha ya kuwa chama kimoja kwa kile kinachotajwa kuwa ni meya huyo
kukataa kutekeleza matakwa ya mbunge huyo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mwenezi wa CCM
wa wilaya ya Kasulu, Masoud Kitowe kuwa mbunge Gezabuke aliwatumia
madiwani wa Halmashauri ya Kasulu kuandika barua kwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Kasulu kuwa hawana imani na meya wa halmashauri hiyo,
Mangu ili meya atolewe katika nafasi hiyo.
Katibu
Mwenezi wa CCM wa wilaya ya Kasulu, Masoud Kitowe akizungumza kuhusu
Mbunge wa Viti Maalum Kigoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),
Josephine Gezabuke kutaka kumtoa madarakani Meya wa Halmashauri ya
Kasulu, Twaribu Mangu.
Kitowe alisema katika barua hiyo
kulikuwa na saini za madiwani 13, 11 wakiwa wa CCM na wawili wakiwa wa
upinzani na baada ya kuwahoji madiwani hao, madiwani sita walisema
walishajitoa katika jambo hilo na hawana hofu yoyote na meya na wengine
watano wakikubali kushiriki na wapo tayari kupewa adhabu na chama.
“Wahusika walipewa onyo kali na
Kamati ya Uongozi na Maadili ya wilaya lakini pia wakiwa katika kipindi
cha uangalizi kwa kipindi cha miezi 18 lakini baada ya kuchunguza nani
yupo nyuma yao tuligunduakuwa mbunge wa viti maalumu Kigoma, Josephine
Gezabure ndiyo anahusika, tulimwita tukamhoji na yeye akapewa adhabu
ambayo mpaka sasa anaitumikia,” alisema Kitowe.
Mbunge
wa Viti Maalum Kigoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Josephine
Gezabuke akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati
alipotembeleaa kijiji cha Nyumbigwa kwa ajili ya kukagua mradi wa maji,
Aprili 9, 2014. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Kigoma, Dk Aman Walid
Kabourou.
Alisema walifanya uchunguzi na kubaini sababu za Gezabuke kutaka meya
wa Kasulu avuliwe madaraka kuwa ni kukataliwa kushiriki vikao vya
Baraza la Madiwani la Kasulu kwasababu alishashiriki kupiga kura katika
Baraza la Madiwani la Kakonko na kukataliwa na meya kumwita Diwani wa
Heru, Avelin Charles katika kikao kutokana na kuwa na mgogoro wao
binafsi, lengo lake ikiwa ni diwani huyo avuliwe udiwani.
“Tunazo sauti anasema kuwa hata
kama tunamzuia lakini mapambano yataendelea na mpaka tunaamua kutoa
taarifa hii tayari tumeshamwambia sana lakini hasikii na anasema ana
watu ngazi za juu na atapanda kwa viongozi wa juu ili hata adhabu
aliyopewa itenguliwe,” alisema Kitowe.
Nae Josephine Gezabure alipotafutwa kwa
njia ya simu ili azungumze kuhusu tuhuma ambazo zinatolewa dhidi yake
hakuwa tayari kuzungumza kwa muda huo.
No comments :
Post a Comment