Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akiwa amewabeba watoto, Editha (kushoto) na Edina wa Kituo cha
kulea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dae es salaam
jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kituo hicho na kutoa misaada
mbalimbali. Desemba 24, 201. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………
MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa makundi ya watoto yatima jijini Dar
es Salaam ili kuwawezesha kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka.
Mama Majaliwa ametoa msaada huo leo
(Jumamosi, Desemba 24, 2016) katika vituo vitatu vya CHAKUWAMA kilichopo
Sinza, HISANI kilichopo Kigamboni na CHAMAZI kilichopo Mbagala.
Akikabidhi msaada huo ikiwemo mchele,
sabuni, mbuzi, juisi na soda, Mama Majaliwa amesema ameona ni vema atoe
msaada huo kwa watoto hao ili na wao waweze kufurahia sikukuu za mwisho
wa mwaka kama ilivyo kwa watoto wengine.
Pia ametoa wito kwa makundi mbalimbali yenye uwezo katika jamii wawe na moyo wa kusaidia makundi yenye uhitaji.
Kwa upande wao, walezi wa vituo vya
kulelea watoto yatima vya CHAKUWAMA na HISANI wamemshukuru mke wa Waziri
Mkuu kwa msaada huo huku baadhi ya watoto wakisema msaada huo umewapa
faraja kubwa.
Mlezi wa kituo cha CHAKUWAMA, Bibi Saida
Hassan mbali ya kushukuru kwa msaada huo, amewaombea kwa Mwenyezi Mungu
awape afya na nguvu za kuendelea kuwatumikia vizuri Watanzania.
Naye Mlezi wa kituo cha HISANI, Bi. Hidaya
Mutalemwa ameiomba jamii iendelee kuyakumbuka makundi yenye uhitaji
kwani bado yanakabiliwa na changamoto nyingi za kufanikisha ndoto zao
ikiwemo kupata elimu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
- L. P. 3021,
11410 – DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, DESEMBA 24, 2016.
Irene K. Bwire
No comments :
Post a Comment