Mkurugenzi
wa Kampuni ya Rabbit Republic ambaye ni mfugaji wa sungura kutoka
Kenya, Moses Mutua (kulia) akielezea mipango yake ya kuzanzisha
machinjio ya kisasa ya sungura hapa nchini, wakati wa hafla ya Kampuni
ya Namaingo kugawa sungura kwa vikundi 20 vya wajasiriamali, Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Donald
Bombo,Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo, Ubwa Ibrahim na Meneja wa Mradi
wa Sungura, Amos Misinde. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Na Richard Mwaikenda;Kamanda wa Matukio Blog
WAKATI
Tanzania ikijielekeza katika uchumi wa viwanda, mpango wa ujenzi wa
machinjio ya kisasa ya sungura yatakayogharimu sh. milioni 100 utaanza
mapema mwakani, ukiratibiwa na Kampuni ya Rabbit Republic.
Mkurugenzi
wa kampuni hiyo, Moses Mutua alisema hayo wakati wa uzinduzi wa ugawaji
wa miradi ya sungura kwa wajasiriamali uliofanywa na Kampuni ya
Namaingo Business Agency jijini Dar es
Salaam wiki iliyopita.
Salaam wiki iliyopita.
Mutua
ambaye ni mfugaji wa sungura kutoka nchini Kenya, alisema uamuzi wa
kujenga machinjio ya sungura unatokana na kuongezeka kwa mwamko wa
wananchi kufuga sungura.
Alisema
awali, mradi huo ulihusisha kusafirisha sungura hai hadi Kenya, lakini
ongezeko la watu wanaohitaji kujishughulisha na biashara hiyo
limesababisha kuwapo haja ya kujenga machinjio
hayo.
hayo.
Alisema nia na uthubutu wa serikali ya Rais John Magufuli kuwaondoa wananchi wanyonge katika
umasikini, ni miongoni mwa mambo yaliyomsukuma kufikia uamuzi huo. “Machinjio hayo yatakayojengwa Dar es Salaam
umasikini, ni miongoni mwa mambo yaliyomsukuma kufikia uamuzi huo. “Machinjio hayo yatakayojengwa Dar es Salaam
yatakuwa
na uwezo wa kuchinja sungura wengi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya
kutenganisha vizuri ngozi, nyama na kucha,” alisema.
Alisema
bidhaa zote hizo zitakuwa zikisafirishwa kuuzwa nje ya nchi ambako
kuna soko kubwa, wakati mkojo na mavi ya wanyama hao yatauzwa nchini kwa
matumizi mbalimbali.
Kwa
mujibu wa Mutua, kampuni yake inakusudia kusafirisha tani mbili za
nyama ya sungura kila siku kwenda kuuzwa nje ya nchi, hivyo kufanya
kiasi kwa mwaka mmoja kufikia tani 720.
Alisema
mbali na sungura, kampuni yake inakusudia kuanzisha hoteli mahsusi kwa
ajili ya uuzaji wa bidhaa zinazotokana na sungura pekee.
Utekelezaji
wa mradi wa sungura kupitia Namaingo, utahusisha mafunzo ya kitaalamu
kwa wafugaji yatakayotolewa kwa ushirikiano na watalaamu kutoka Suma JKT
na Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Donald Bombo alisema hatua
iliyofikiwa na Mkurugenzi wa Namaingo, Ubwa Ibrahim kuanzisha mradi huo
ni ya ujasiri na uthubutu unaolenga kuwanufaisha wananchi na kuinua
vipato vyao.
Bombo aliahidi kuwa, serikali itakuwa bega kwa bega kuhakikisha mipango ya kusaidia kiuchumi wananchi inafanikiwa.
Alisema
ujenzi wa machinjio ya kisasa ya sungura unadhihirisha umoja na
ushirikiano thabiti wa wafanyabiashara katika nchi wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC).
wajasiriamali wa Mkoa wa Dar es Salaam
No comments :
Post a Comment