Thursday, December 1, 2016

IRELAND HELPS MAINTAIN CRITICAL SUPPORT TO REFUGEES IN TANZANIA



At the refugee camps pregnant and nursing women as well as children under the age of five receive supplementary nutritious foods which can help in the fight against undernutrition.
Refugees in Tanzania receive a food basket from WFP including maize meal, pulses, salt, vegetable oil and fortified porridge mix.
A father and his children enjoy lunch cooked with food from WFP’s food basket at Nyarugusu Refugee Camp.(PHOTO:
COURTESY OF WFP)


 
Tanzania security officer, (R), screens the arrival refugees from Burundi, at Kigoma port early 2015.(PHOTO; LIBRARY)

Ireland helps maintain critical support to refugees in Tanzania


Mshauri Mwelekezi wa Masuala ya Jinsia kutoka “Women Fund” Profesa Ruth Meena akitoa mada.

 Mshauri Mwelekezi wa Masuala ya Jinsia kutoka “Women Fund” Profesa Ruth Meena (kulia), akiwasilisha mada juu ya jinsi ya kuingiza masuala ya jinsia katika mpango kazi wa taasisi wakati wa kikao kazi cha watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilicho fanyika leo katika Ukumbi wa ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
 Mafunzo yakitolewa.

 Diwani wa kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Shirika la Eguality for Growth (EfG), Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele na kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mchikichini, Charles Kapongo.

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki amezindua shughuli ya kupanda miti maeneo oevu/ kwenye vyanzo vya Maji katika Kata ya Bwambo. Zoezi hilo limefanyika kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la Floresta.






BARAZA la madiwani  Halmashauri ya Meru mkoani Arusha wamkaanga Mkurugenzi wasema hana uwezo wa kuongoza  Halmashauri hiyo.


Akitoa  maazimio  ya kikao  cha baraza kilichokaa siku mbili kilichowajumuisha  madiwani,wakuu wa idara mbalimbali na wataalam Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Willy Njau Alisema wametafakari kwa kina utendaji wa Mkurugenzi na kubaini kuwa hafai.


" Tumejadili ajenda ya utendaji  usioridhisha wa Mkurugenzi wetu na tumeona  kuwa haufai kutokana na mambo mengi anayoyafanya yanakiuka kanuni na taratibu za Halmashauri"alisema Njau.


Aidha Njau alisema Mkurugenzi huyo ameonekana kukata mawasiliano na mwenyekiti wa Halmashauri jambo alilosema siyo sahihi.


Alisema pia ameweza kukata mawasiliano na madiwani wa Halmashauri hiyo pamoja na kusababisha hata wakuu wa idara kutokuwa na mawasiliano na madiwani jambo linalorudisha maendeleo nyuma.


Aliongeza kuwa Mkurugenzi huyo ameshindwa kukusanya makusanyo ya pesa kiasi cha milioni 150 kilichokusudiwa kukusanywa  tangu  Julai hadi septemba mwaka huu jambo alilosema linaweza kusababisha Halmashauri kutopewa ruzuku kutoka serikali kwasababu  ya uzembe.


" Tumejiridhisha kuwa uwezo wa Mkurugenzi kuiongoza Halmashauri yetu kama Mkurugenzi Mtendaji ni mdogo hivyo hafai anadidimiza maendeleo ya Halmashauri ya meru" alisema Njau. Na kuongeza.


"Tumeamua kuiomba mamlaka yake  na Uteuzi ichukue  hatua stahiki za kumuwajibisha ili kunusuru maendeleo ya Halmashauri ya meru"


Vilevile alisema  kuwa  Mkurugenzi huyo amekuwa  akidharau maagizo yanayotolewa na  kamati mbalimbali za baraza hilo na Kushindwa kuzitekeleza ambapo ni kuvunja kanuni na taratibu za Halmashauri.


Hata hivyo alisema kitendo cha mkurugenzi kukata posho zamadiwani ni kinyume na utaratibu kwani ziliwekwa kisheria ambapo alisema  Kama kuna tatizo la kukatwa  posho ni lazima sheria hiyo ingebadilishwa kwanza.


" Mwenye dhamana ya kutangaza kuwa posho zinabadilika ni Waziri mwenye dhamana hiyo  lakini siyo mkuu wa mkoa, Wilaya au Mkurugenzi" alisema .

Naye Diwani wa Kikatiti  Elisa Mungure ambaye ni Mwenyekiti wa madiwani alisema Mkurugenzi huyo amekuwa  akiendesha Halmashauri kisiasa jambo ambalo halifai.


" Ninasikitishwa na uongo unaoelezwa na Mkurugenzi ambaye kateuliwa na mheshimiwa Rais hii ni ajabu haiwezekani kuendelea kumuamini mtu wa aina hii" alisema Mungure.


Alisema Mkurugenzi huyo amekuwa  akiwqhamisha watendaji wa kata  bila  kufuata taratibu huku akishinikiza ofisi ya kata ya Kikatiti kuwa ni ya CCM  huku ikiwa ni ofisi ya wananchi wala siyo ya chama chochote.


Kwa upande wake mkurugenzi  Huyo Christopher Kazer  alisema anafuata maagizo ya mkuu wa nchi na hawezi kuwanyima watu kufikiri  wanavyofikiri.


" Maelekezo ya kupunguza matumizi yasiyolazima kutoka kwa mkuu wa nchi ninayafuata pia ndio maana nimepunguza matumizi mengi" alisema.


Alisema hawezi kuzuia maamuzi yanayotolewa na baraza hilo maana kwa namna moja au nyingine wamekaa wakatengeneza maamuzi hivyo hawezi kuwalazimisha kutofanya maamuzi.

Aidha pia alibainisha kuwa anaamini kabisa madiwani hawa wanataka halmashauri iendeshe kisiasa wanataka iendeshwe kama wao wanavyotaka kitu ambacho hatakubali kwani sio hakutumwa kufanya kazi ya siasa bali alitumwa kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi na serikali kwa ujumla 

Alisema kuwa anaamini haya yote yanatokea kutokana na madiwani hawa kukatwa fedha za posho na usafiri ambao walikuwa wamejiwekea bila kufuata taratibu

"ivi jamani ndugu waandishi mtu anatoka apo usa anataka alipwe nauli elfu 80 ni haki kweli wengine wanatoka apa apa wakija kikao kikichelewa kuisha wanataka walipwe  fedha za kulala laki laki sasa mimi hayo yote tumeyatoa sasa ivi wanalipwa elfu 40 tu na mshahara wao upo pale pale sasa wao ndio maana wananipiga zwegwe mimi nasema nitasimamia ilani ya chama ambacho kinaongoza serikali pia nitafata sera ya muheshimiwa Rais ya kubana matumizi sitakubali  wafanye vitu ovyo na ninyamaze walifikia atua wakataka hata kunigombanisha na watendaji wangu ila mimi nimeajiriwa na serikali mimi sio mwanasiasa na nitafanya kazi kama nilivyoaaidi siku nilioapishwa "alisema mkurugenzi  Kazer
 Makamu mwenyekiti wa baraza la madiwani Meru akiwa anachangia hoja katika baraza hilo
 Baadhi ya madiwani wa meru wakifuatilia kikao
 Mkurugenzi   wa halmashauri ya Meru  Christopher Kazer akifafanua jambo kwa waandishi mara baada ya baraza kumalizika
  Mkurugenzi   wa halmashauri ya Meru  Christopher Kazer akijibu hoja mbele ya madiwani wa meru
     (Habari picha na  Woinde Shizza-Arusha)


Meya wa jiji la Mbeya David Mwasilindi


 Na JamiiMojablog,Mbeya
Halmashauri ya jiji la Mbeya imebuni njia mpya ya ukusanyaji wa mapato  ili kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa kiasi cha shilingi bilioni  11 katika  mwaka wa fedha wa  2016/17 .
Katika kufanikisha mpango huo halmashauri imewashirikisha madiwani na wataalmu wake katika kufanya kazi ya ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani .

Moja ya njia hiyo halmshauri imeanza kuwatumia Madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa katika ukusanyaji wa fedha kupitia vyanzo vyake vya ndani vya mapato .
Akielezea mkakati huo  Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Ndugu David Mwashilindi amesema katika kuhakikisha halmshauri inafikia lengo lake la ukusanyaji wa mapato imeamua kuongeza nguvu kazi kwa kuwaingiza madiwani na wenyeviti ambao wapo karibu na wananchi.

Kazi kubwa  wanayo ifanya madiwani na wenyeviti kwa kushirikiana na wataalam ni kuhakikisha wanavitambua vyanzo vyote vya mapato vinavyostahili kuingia katika mapato ya halmashauri  ikiwa na kubaini mianya iliyokuwa ikitumiwa na wahusika kukwepa kulipa kodi,”amesema Mwasilindi.

Amesema kuziendesha halimamshauri hizi inategemea sana mapato ya ndani hivyo lazima kuweka jitahada za makusudi katika kufikia malengo husika .

Amesema katika kipindi cha nyuma halmasahuri hiyo hali ilikuwa katika hali mbaya kwani kwa mwezi walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi milioni 120 hadi 200 lakini mara baada ya kuanza kwa jitihada hizo imesaidia kupandisha mapato ambapo kwa sasa imefikia kiasi cha shilingi milioni 700 kwa mwezi.

Amesema zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo sanjali na kukusanya mapato pia kuna sauala la utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuelewa namna ya kulipa  tozo zilizo wekwa kisheria.

Amesema zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku tano na mara baada ya hapo kutafanyika kwa tahimini ya pamoja ili kubaini changamoto zilizopo katika zoezi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, wakielekea eneo ambalo lilitumika kufanya ibada ya kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda, baba mzazi wa Waziri Mkuu mstaafu Pinda, huko Zuzu mkoani Dodoma leo Novemba 30, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kushiriki katika kuaga mwili wa Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu Marehemu, Xavery Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Zuzu, Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakiwa nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Zuzu, Manispaa ya Dodoma ambako walishiriki katika kuaga mwili wa baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Xavery Mizengo Pinda Novemba 30, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama  akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Angela Kairuki   akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016

Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda  kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016
Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda  kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akipewa pole na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa wakati awa kuaga mwili wa Baba yake mzazi wa Waziri Mkuu mstaafu,  marehemu, Xavery Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispa ya Dodoma Novemba 30, 2016
Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akizungumza wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa Marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016
Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akizungumza wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa Marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016

Waziri Mkuu, KassimMajaliwa akizungumza na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda baada ya kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda baada ya kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wapili kulia ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene


Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu baba yake, Xavery Mizengo Pinda kijijini kwake Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016


Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  akizungumza wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa Marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kijijini

No comments :

Post a Comment