Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan
Chandra Acharya (kulia) akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango (hayupo pichani) kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Umoja
huo, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Wajumbe walioshiriki mazungumzo
kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) anayeshughulikia
masuala ya Nchi Masikini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (wa pili
kulia), ambapo masuala kadhaa yakiwemo maendeleo ya Sekta Binafsi na
Miundombinu yalijadiliwa kwa kina wakati ujumbe huo kutoka UN
ulipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Ofisini kwake Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa kwanza kushoto), akielezea mpango wa
Serikali wa kutumia malighafi za ndani katika kufikia maendeleo ya
viwanda nchini, katika Kikao kati yake na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi Masikini Duniani Bw.
Gyan Chandra Acharya (wa kwanza kulia), Mazungumzo yaliyofanyika Makao
Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Wajumbe walioambatana na Msaidizi
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan
Chandra Acharya, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) alipokuwa akielezea umuhimu wa amani katika maendeleo
ya Bara la Afrika, wakati wa kikao chake na Kiongozi huyo katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi Maskini Duniani Bw.
Gyan Chandra Acharya (kulia) akisikiliza kwa makini maelezo ya Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani),
alipokuwa akielezea miradi itakayowakwamua wananchi kiuchumi ikiwemo ile
ya Kilimo itakayosaidia kuendesha viwanda. Mazungumzo hayo yamefanyika
Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kushoto), akifurahia jambo wakati Msaidizi
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Nchi
Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (hayupo pichani), akielezea
ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa, wakati wa
kikao kilichofanyika Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini
Dar es salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
No comments :
Post a Comment