Mkulima mdogo mdogo wa matikiti mwanadada Annie Nyaga kutoka Kenya,
ambaye ni msomi aliyemaliza digrii ya kwanza ya biomedical science and
technology, anasema kilimo ndiyo ndoto yake aliyoipoteza miaka minne yote ya
chuo kikuu. Anasema kwa sasa kilimo ndiyo kazi anayopendelea kuliko kazi nyingine
yeyote.
Taarifa za idadi ya watu
nchini zinaonesha kuwa asilimia 44.4 ya Watanzania wote wana umri chini ya
miaka 15. Hili ni kundi lingine kubwa mno la Vijana watarajiwa ambao inabidi
kuwaandaa kama nguvukazi ya Taifa letu.
Pamoja na mafunzo ya ujasiriamali
yanayotolewa, vijana na wanachama inatakiwa wawezeshwe na kuwekewa mifuko ya
uwezeshaji yenye utaratibu maalum ulio wazi na mwepesi wa kupatikana kwa
mikopo.
Kwa mujibu wa takwimu za
hivi karibuni zinaonyesha kuwa wastani wa nguvukazi hasa vijana wasomi
wanaotafuta ajira kwa mwaka ni takriban 800,000 hadi 1,000,000. Hata hivyo,
ajira rasmi zinazopatikana nchini katika sekta ya umma na sekta binafsi ni
kidogo, takriban ajira 80,000 hadi 100,000 kwa mwaka.
Takwimu pia zinaonyesha kuwa
kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 wanakadiriwa kufikia
milioni 8.3, sawa na asilimia 19.8 ya watanzania. Vijana wasomi ndiyo wapo
kwenye kundi hili. Vijana wengine watarajiwa ni wale walio kwenye umri chini ya
miaka 15.
Miongoni
mwa changamoto kubwa ambayo Vijana wengi wajasiriamali wanaopenda kujiajiri
wanakumbana nayo ni ukosefu wa mitaji na mikopo yenye masharti nafuu. Taasisi
nyingi za fedha nchini na benki za biashara zinatoa mikopo kwa riba kubwa na
masharti mengi, ambayo vijana na wanachama wa mifuko wengi hawawezi kuyamudu.
Mifuko inatakiwa kusaidia
kuleta maendeleo kwa nchi kwa kuchangia kuanzisha miradi mbalimbali ambayo
inaweza kuajiri vijana ambao kama asilimia 90 ya vijana wa kitanzania hawana
kazi na kusaidia vijana wajasiriamali kuanzisha miradi yao ambayo baadaye
husaidia tena kuajiri baadhi vijana wengine. Idadi ya watanzania mpaka sasa
imefikia milion 45 na asilimia 63 ya nguvukazi ni vijana.
Tatizo kubwa linalowasumbua
vijana ni ukosefu wa ajira. Hivyo mifuko inatakiwa kuwa na malengo ya makusudi
ya kuhakikisha kuwa inakuwa na miradi mbalimbali ambayo itasaidia vijana wa
kitanzania kupata kazi kuajiriwa au kujiajiri wenyewe. Vijana wanatakiwa kuwa
wajasiriamali wazuri wenye ujuzi mbalimbali, na kuwa wavumbuzi na wabunifu wa
vitu mbalimbali vitakavyoweza kukuza uchumi wetu.
Lakini ieleweke wazi ya kuwa
lengo la mifuko hii ya hifadhi ya jamii ni kwa ajili ya kumsaidia mfanyakazi
kumudu mahitaji yake ya uzeeni pindi anapostaafu ili kumsaidia uzeeni kwani
ilibainika kuwa wakati wa ujana, wafanyakazi wengi hushindwa kujiwekea akiba ya
kutosha wao wenyewe.
Mifuko ni kama ilivyo sera
ya bima yaani mtu hulipwa pale anapopatwa na janga, na mahususi kumsaidia
mfanyakazi kununua vitu vya thamani kama vile viwanja au kujenga nyumba
anapostaafu au anapoelekea kustaafu.
Kutokana na umuhimu huo
mifuko inatakiwa kuwasaidia vijana na wanachama jinsi ya kuanzisha miradi
mbalimbali wakati bado wapo kazini kwa kutoa mikopo ya gharama nafuu kabla na
pale wanapostaafu.
Mifuko hutoa malipo ya
mkupuo wa pensheni ya asilimia kadhaa ili kuanzisha miradi ya aina mbalimbali
kwa kusaidiwa na wataalamu kutoka katika mifuko hiyo hiyo ya hifadhi ya jamii
hasa kwa kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uanzishwaji na uendesheshaji wa
miradi.
Lengo iwe kutoa huduma zote
muhimu pale wanachama na familia zao wanapopatwa na majanga ya aina mbalimbali
ambayo kwa sasa yamekuwa yakitokea mara kwa mara yakiwemo majanga yanayosumbua
wanachama kiuchumi na kijamii.
Mifuko hii inatakiwa
kuhahakikisha kuwa vijana na wanachama wake wanaopatiwa mikopo ya gharama nafuu
wanapata elimu ya ujasiriamali ya kutosha kwa kushirikiana na taasisi husika
ili wajue malengo ya mikopo ya biashara na hata pia kuelemishwa juu wajibu wao
kwenye mifuko, wajibu wa mwajiri, mafao yatolewayo na mifuko hii, jinsi ya
kuwekeza na kwa nini michango yao inawekezwa na faida ya riba wanayopata
kutokana uwekeza
Mifuko
inatakiwa kuwa na mbinu za ubunifu wa hali ya juu hasa kwa kufanya utafiti kwa
kwenda mbele zaidi kwa kuwatumia mawakala mbalimbali ambao wanaweza kutumika
kuwaandikisha wanachama kutoka katika sekta isiyo rasmi na walioko ughaibuni na
hata katika utoaji wa mikopo ya riba nafuu kwa wanachama
Hatimaye
kwa kufanya hivyo itasaidia hata kujenga mshikamano zaidi sehemu za kazi, na
kuwasaidia waajiri kuongeza uzalishaji wenye tija zaidi na hivyo kusaidia
msukumo wa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati muafaka,
kuwapunguzia ukali wa maisha wanachama na hivyo kupunguza umasikini kama sio
kuondoa kabisa,
Hifadhi ya jamii imeundwa
kwa ajili ya kuwapatia mfanyakazi ulinzi dhidi ya majanga ya kiuchumi na ya
kijamii yanayosababishwa na kukoma au kupungua kipato kutokana na maradhi,
uzazi, kuumia kazini, ukosefu wa ajira, ulemavu, uzee, kifo na kuongezeka kwa
gharama za matibabu.
Hifadhi ya jamii ni kwa
ajili ya manufaa ya kumkinga mfanyakazi dhidi ya majanga. Na ili kuwepo na
hifadhi ya jamii ambayo ni kinga lazima ichangiwe fedha. Kwa ukweli ni kwamba
hifadhi ya jamii inachangiwa na michango kutoka kwa mwajiri na mfanyakazi
pamoja au kujichangia mtu mwenyewe aliyejiajiri au mfanyakazi aliyeajiriwa kwa
mfumo wa hiyari
No comments :
Post a Comment