Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM
,Kibaha Mjini wakifuatilia jambo katika kikao cha halmashauri hiyo
kilichokaa ili kujiwekea mikakati ya ushindi katika uchaguzi mdogo wa
kata ya Misugusugu,ambapo desemba 31 /2016 CCM inatarajia kuzindua
kampeni zake rasmi.(picha na Mwamvua Mwinyi)
..
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
CHAMA cha Mapinduzi(CCM) Kibaha
Mjini ,kimejipanga kushinda katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya
Misugusugu ambapo chama hicho kinatarajia kuzindua rasmi kampeni zake
des 31 mwaka huu.
Uchaguzi huo unarejea kwasababu
march 31/ 2016,mahakama ya mkoa wa Pwani ilitengua uteuzi wa diwani wa
chama hicho Addhudad Mkomambo ambae alishinda katika uchaguzi mkuu
uliopita.
Aidha katika uzinduzi huo mwenyekiti wa CCM mkoani Pwani,Mwinshehe Mlao anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Katibu wa CCM Kibaha
Mjini,Abdallah Mdimu ,aliyasema hayo katika kikao cha halmashauri kuu ya
CCM wilaya ,kilichokaa ili kujiwekea mikakati madhubuti ya kupata
ushindi kwenye uchaguzi huo.
Alieleza kwamba uchaguzi huo
ulitenguliwa kutokana na namba saba kuzidi kwa hesabu kati ya waliopiga
kura na kura walizopata wagombea wa vyama vyote hivyo mahakama kufanya
maamuzi hayo ili kujiridhisha.
“Wapiga kura wote walikuwa
4,830,waliopiga kura 3,191,huku katika matokeo CCM ilipata kura
1,545,chadema 1,525,ACT 66 na CUF 55 “
“Ambapo kura saba hazikujulikana
ni za nani kati ya zilizopigwa na matokeo hivyo mahakama kuamua kutengua
ushindi wa awali”alisema Mdimu.
Mdimu alisema chama hicho
kimejipanga vizuri na tayari wameshazunguka katika matawi yote nane
yaliyopo katika kata hiyo ili kuhakikisha kiti hicho kinarudi kwa CCM.
Hata hivyo ,katibu huyo
alisema ,mgombea mteule wa nafasi ya udiwani kupitia CCM katika kata ya
Misugusugu,amechaguliwa kuwa ni Ramadhani Bogas ambae alishinda katika
kura za maoni na kisha kupitishwa kwenye vikao mbalimbali vya wilaya na
mkoa .
Alibainisha kuwa Ramadhani Bogas
hivi karibuni alishinda kwenye kura za maoni zilizopigwa ndani ya chama
hicho na kuwashinda wenzie saba ambao walijitokeza kugombea akiwemo
diwani wa awali wa kata hiyo Addhudad Mkomambo .
Nae katibu wa CCM mkoani
Pwani,Haji Hassan Mtenga,aliwataka wanachama wa chama hicho kuwa wamoja
na kuondoa makundi yasiyo na tija ndani ya chama.
Aliwaambia kwamba ni wakati wa kutunza wajibu wao kwa ajili
ya kushika dola na kuondokana na tofauti zao ambazo wakati mwingine
huzaa maumivu .
Mtenga aliziomba jumuiya zote
ziungane pamoja kujenga mipango na mikakati itakayowasaidia kuvuka
katika uchaguzi huo mdogo na kupata ushindi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM
Kibaha Mjini,Maulid Bundala aliwaomba wananchi hususan vijana kujiokeza
kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni hizo sambamba na kumpigia kura
mgombea kupitia CCM siku ya kupiga kura.
Aliwataka wanaCCM kuacha kujibweteka na kusubiri ushindi uje miguuni pasipo kupigana kufa na kupona ili ushindi upatikane.
“Hapa ni kazi kazi,ipo kazi ya
ziada ya kufanya ,kumbukeni hakuna ushindi unaokuja kwa kubahatisha na
hakuna mashindano rahisi,tusidharau tupambane kwa lengo la kurejesha
nafasi hiyo mikononi mwa CCM”alisema Bundala.
Bundala alisema maendeleo
yanapatikana ndani ya chama kubwa CCM ,na haina ubishi ,kwani kila mmoja
naona namna serikali ya awamu ya tano kupitia CCM inavyofanyakazi na
kuinua uchumi kwa kasi nchini.
No comments :
Post a Comment