Tarehe
1 Desemba kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani,mwaka huu
2016 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya dhahabu ya Acacia kupitia mgodi wa
Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeadhimisha siku hiyo
kwa kuzindua Mashindano ya mpira wa miguu na pete “Mahusiano Cup” ili
kuhamasisha jamii inayozunguka mgodi huo kupima virusi vya Ukimwi.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mahusiano yaliyoenda sambamba na
zoezi la upimaji wa VVU katika uwanja wa taifa mjini Kahama , Meneja
mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo alisema kampuni yao
inazidi kufarijika kuona namna mahusiano baina ya mgodi na wananchi
wanaozunguka mgodi huo.
“Mahusiano na jamii yamekuwa
yakiimarika siku hadi siku,awali tulipoanza mashindano haya mwaka 2009
ni kata ya Mwendakulima pekee ndiyo ilikuwa ikinufaika kwa kuzikutanisha
timu zinazounda mitaa yake ambayo ni Mwime,Chapulwa,Busalala na
Mwendakulima”,alisema Mhandisi Mwaipopo.
Mhandisi Mwaipopo alisema mashindano hayo yataendelea hadi Desemba 8 mwaka huu yakikutanisha timu 14 za mpira wa miguu na timu 6 za mpira wa pete.
Mhandisi Mwaipopo alisema mashindano hayo yataendelea hadi Desemba 8 mwaka huu yakikutanisha timu 14 za mpira wa miguu na timu 6 za mpira wa pete.
“Timu zote 20 zimekabidhiwa
jezi na mipira vyote vikiwa na gharama ya shilingi 20,355,000/=,kwa timu
ya mpira wa miguu na pete mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya shilingi
400,000/= na kombe,mshindi wa pili 300,000/= na mshindi na kwa upande
wa kampeni ya utoaji elimu ya Ukimwi jumla ya shilingi 25,600,000/=
zimetumika kununulia vifaa vya upimaji na uendeshaji wa zoezi
lenyewe”,aliongeza Mhandisi Mwaipopo.
Alisema kwa kubadilisha mtazamo wa uendeshaji wa michezo ya mahusiano Cup awamu hii wamezihusisha kata nyingi zaidi za tarafa ya Kahama Mji na itakuwa fursa muhimu kwa wadau wa michezo kuweza kuona vipaji vya wanamichezo na kutafuta namna nzuri ya kuviendeleza.
Alisema kwa kubadilisha mtazamo wa uendeshaji wa michezo ya mahusiano Cup awamu hii wamezihusisha kata nyingi zaidi za tarafa ya Kahama Mji na itakuwa fursa muhimu kwa wadau wa michezo kuweza kuona vipaji vya wanamichezo na kutafuta namna nzuri ya kuviendeleza.
Alizitaja timu za mpira wa
miguu zitakazoshiriki kuwa ni Nyihogo,Nyahanga,Busoka,Kahama
mjini,Zongomela,Malunga,Majengo,Mwendakulima,Ngogwa,Nyasubi,Mhongolo,Wendele
na timu ya mgodi wa Buzwagi na timu za mpira wa pete kuwa ni Kahama
mjini,Mhungula,Mwendakulima,Mhongolo,Ngogwa na Zongomela.
Katika hatua nyingine mhandisi
Mwaipopo alisema kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi vimeshuka
katika mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi wilayani Kahama mkoani
Shinyanga kutoka asilimia 2.6 mwaka hadi kufikia asilimia 0.4 mwaka 2016
baada ya kuwahamasisha kupima afya zao.
Mwaipopo alisema pamoja na
kiwango cha ndani ya mgodi kuridhisha maeneo yanayozunguka mgodi wa
Buzwagi yana kiwango cha juu cha maambikizi ya VVU ambapo takwimu
zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizi kwa wilaya ya Kahama kwa takwimu
za kitaifa ni asilimia 9.6,mkoa wa Shinyanga asilimia 7.4.
Naye mkuu wa wilaya ya Kahama
Fadhili Nkurlu aliupongeza mgodi huo kwa kuchukua hatua ya kuhamasisha
jamii kupima VVU kupitia michezo kwani takwimu za maambukizi zinatisha
wilayani humo ambapo asilimia 70 ya vijana wenye umri kati ya miaka 20
hadi 49 wamepata maambukizi ya VVU,ambao ndiyo nguvu kazi ha taifa.
Nkurlu aliupongeza mgodi huo
kwa kuwa mdau mkubwa wa michezo wilayani humo kwa kudhamini timu kadhaa
na kuziwezesha kushiriki katika mashindano mbalimbali ndani nan je ya
mkoa wa Shinyanga.
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (katikati) akisindikizwa na meneja
mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo kwenda kukagua timu
zinazoshiriki Mahusiano Cup mara baada ya kuwasili katika uwanja wa
taifa wa Kahama.Kulia ni Meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mkanza
na wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya
ya Kahama Ibrahim Khan akifuatiwa na mkuu wa polisi wilaya ya Kahama
Kulia
ni afisa mawasiliano na habari wa mgodi wa Buzwagi bwana Magesa Magesa
(mwenye shati la bluu) akiongozana na maafisa wa serikali walipowasili
uwanjani. Kushoto kwake ni katibu tawala wilaya ya Kahama Timoth Ndanya
,Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba pamoja na
maafisa wengine wa serikali
Washiriki wa Mahusiano Cup wakiwa uwanjani wakisubiri kukaguliwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Nyihogo
No comments :
Post a Comment