Monday, November 28, 2016

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Mwakyembe afanya ziara mkoani Mbeya

index
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe yuko mkoani Mbeya kuangalia utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara yake na kuzungumza na watendaji ndani ya taasisi hizo

Katiba Ziara hiyo Dkt Mwakyembe alianza kwa kutembelea kituo cha usajili watoto chini ya umri wa miaka mitano na kupatiwa cheti cha kuzaliwa kilichopo Katiba jiji la Mbeya
Akizungumza katika kituo hicho Dkt Mwakyembe ameutaka uongozi wa mkoa wa Mbeya kuhakikisha zoezi hilo la usajili watoto Ili wapatiwe vyeti vya kuzaliwa linakuwa na mafanikio kama ilivyo katika Mikoa ya Iringa na Njombe ambayo imeandikisha watoto wao kwa asilimia 98 ndani ya miezi miwili tangu mpango huo uzinduliwe katika mkoa wa Iringa mwezi Septemba Mwaka 2016
Amesema usajili wa watoto hao na raia wengine kunaiwezesha nchi kupanga kikamilifu mipango yake ya maendeleo kwani itaiwezesha nchi kuzingatia mahitaji husika kwa mujibu wa takwimu zilizopo.
Akiwa Mahakama Dkt . Mwakyembe amewapongeza Majaji na Mahakimu kwa kujitoa Kwao na kufanikisha azma ya upunguzaji wa mlundikano wa kesi uliokuwa ukiikabili Mahakama ndani ya  kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Amesema kiwango walichojiwekea Majaji na Mahakimu kimesaidia sana kufanikisha suala la mlundikano wa mashauri ya wananchi yaliyopo mahakamani yanamalizwa na mengine kwa wakati.
Dkt Mwakyembe pia alitembelea Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani humo na kuzungumza na wafanyakazi wa ofisi hiyo na kuwapongeza kwa kazi kubwa ya kuitetea Serikali Mahakamani wanayoifanya na kuwaeleza kuwa Serikali ya awamu ya Tano inathamini mchango wao mkubwa wanaoutoa na kuokoa Mali na fedha za umma.
Waziri Mwakyembe pia ametembelea gereza la Ruanda la mkoani Mbeya na kuzungumza na maafisa wa Jeshi la Magereza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo

No comments :

Post a Comment