Sunday, November 20, 2016

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA ZIFF AZINDUA TAMASHA LA UONESHAJI FILAMU BURE MKOANI GEITA.


Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye.

Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Desire Park Geita ambapo Taasisi ya Sanaa Na Mazingira ya Kijani Consult Tanzania imeanzisha kampeni ya kuonesha bure Filamu mbalimbali kwa ajili ya kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya Utunzaji wa Mazingira (Mabadiliko ya Tabianchi), Ufugaji wa kuku wa kienyeji, Usalama barabarani, Madawa ya kulevya, Madhara ya ndoa za utotoni miongoni mwa mambo mengi ya kijamii. Mradi huo umefadhiriwa na ZIFF.

Kutokana na Mwitikio wa wanatasnia ya Filamu mkoani Geita kuonesha shauku ya kuwa na Maonesho hayo ya Filamu, Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
Na BMG
Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo, akizungumza kwa niaba ya Serikali kwenye uzinduzi huo ambapo aliwahakikishia Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na nchini kwa ujumla kwamba Serikali itahakikisha inaboresha zaidi sanaa ya filamu ikiwemo kuendelea kutoa mafunzo ya filamu kwa wanatasnia hiyo ili filamu zinazozalishwa ziwe na ubora.
Aidha alidokeza kwamba Serikali inatoa baraka zote kuhusiana na Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar, pia kufanyika mkoani Geita hapo mwakani.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Uoneshaji wa Filamu mkoani Geita, ambapo alisisitiza kwamba sanaa ni ajira hivyo wanatasnia hiyo watumie fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo yanayotolewa na serikali ili kuboresha zaidi kazi zao.
Katibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Robert Manondolo, akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo alibainisha kwamba ZIFF imekuwa ikitoa ufadhiri kwa taasisi mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Kijani Consult kwa lengo la kuziwezesha kufikisha elimu kwa umma kwa njia ya kuonesha filamu bure na kufikisha elimu iliyokusudiwa.
Katibu Tawala Wilayani Geita, Thomas Dimme, akizungumza kwenye uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu bure mkoani Geita ili kufikisha elimu mbalimbali ikiwemo Ufugaji na utunzaji wa Mazingira.
Herman Matemu (aliyesimama) ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita, akisalimia kwenye uzinduzi huo.
Kulia ni Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani Geita, akisoma risala kuhusiana na Mradi wa Uoneshaji Filamu Bure mkoani Geita.
Alisema mradi huo umelenga kutoa chachu kwa wanajamii kutumia fursa mbalimbali ikiwemo ufugaji kujipatia kipato badala ya kutegemea shughuli moja kama vile madini. Pia kuwahimiza kujiepusha na uharibifu wa mazingira. Yote hayo pamoja na mengine yanafikishwa kwa wananchi kwa njia ya filamu.
Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (kulia) akipokea taarifa ya mradi wa uoneshaji wa filamu bure mkoani Geita kutoka kwa Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani Geita (kushoto).
Mkuu wa idara ya Habari, Kijani Consult Tanzania, Rose Mweko, akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure katika maeneo ya wazi mkoani Geita.
Kutoka Kushoto ni Mwakilishi wa Balozi wa Denimark nchini Tanzania, Dotto Kahindi, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo na Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, wakifuatilia kwa makini zoezi la uzinduzi wa mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita ili kufikisha elimu kuhusu masuala mbalimbali kwa wanajamii.
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi wa mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita
Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo
Maafisa Habari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wageni mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wanahabari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wanatasnia wa Filamu mkoani Geita
Burudani za asili mkoani Geita
Burudani za asili zikiendelea
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Geita wakifuatilia Uzinduzi wa Mradi wa Uoneshaji wa Filamu bure mkoani humo ili kufikisha elimu ya masuala mabalimbali ikiwemo uharibifu wa mazingira pamoja na ufugaji kwa njia ya filamu
Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (mwenye kofia) pamoja na viongozi wengine, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto walioshiriki shindano fupi la kucheza muziki kwenye Uzinduzi wa Mradi wa kuonesha Filamu bure mkoani Geita.
Mgeni Rasmi Mhe.Kombo (mwenye kofia) pamoja na viongozi wengine, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto, Maisala Ibrahimu anayesoma kidato cha pili shule ya Sekondari Kangalala (ke) na Joshua Tito anayesoma darasa la kwanza shule ya msingi Kivukoni Geita (Me) ambao walioonesha vipaji vya hali ya juu katika kucheza muziki. 
ZIFF imetoa fursa ya kuwanunulia mavazi ya shule watoto hao huku pia wakipata fursa ya Kuhudhuria Tamasha la Kimataifa la Filamu katika Visiwa vya Zanzibar hapo mwakani.
Bonyeza HAPA Kutazama picha za kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na Bodi ya Filamu Tanzania.


 Wanafunzi waliohitimu na kutunukiwa Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakishangilia wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick  Shoo, alitunuku  jumla ya wahitimu 733. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG}
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick  Shoo,akimtunuku Evelyn Wallace Shundi Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
 Wahitimu Agnes Nsokolo (kulia) na Asha Kidendei wakiwa na furaha baada ya  kuwa miongoni mwa wahitimu 43 waliotunukiwa  Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
 Evelyn Shundi ambaye ni mfanyakazi wa Ewura akiwa na furaha wakati wa mahafali hayo.
 Wahitimu wakivaa kofia baada ya kutukiwa
 Mmoja wa wanafunzi akipatiwa cheti wakati wa mahafali hayo
 Wakivaa kofia ikiwa ni ishara ya kunukiwa
 Wahitimu wakiwa wamekaa baada ya kutunukiwa
 Wahitimu wakiwa wamesimama mbele ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakisubiri kutunukiwa Shahada ya Uzamili
 Domina Rwemanyila (kushoto) na Diana Tengia wakiwa na furaha baada ya kutunukiwa Sahada ya Sanaa ya  Mawasiliano ya Umma
 Ni furaha iliyoje kutunukiwa Shahada ya Uzamili
 Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Dk Frederick Shoo na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu waliotunukiwa Sahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara
 Wapigapicha wakiwa kazini wakati wa mahafali hayo
 Brass Band ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakipiga wimbo wa Taifa wakati wa kuhitimisha mahafali hayo
 Julieth (katikati) akiwa na ndugu zake baada ya kuhitimu katika chuo hicho. KWA MAWASILIANO ZAIDI;0715 264202/0754 264203




Bw. Bernard Mchomvu, ambaye Rais John Pombe Magufuli, ametangaza kutengua uteuzi wake kama Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya  Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA)



Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (kushoto) pamoja na mkuu wa chuo hicho Prof. Innocent Ngalinda (kulia) kuingia ukumbini pamoja na wahitimu tayari kwa mahafali.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua mahafali ya pili yaliofanyika chuoni hapo.
Sehemu ya Wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku mmoja wa wahitimu kati ya wahitimu 133 waliohitimu leo na kutunukiwa Shahada na Stashahada.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Sudan Mhe.Mahgoub Ahmed Sharfi , ambapo mabalozi mbali mbali walihudhuria.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Mabalozi wa nchi mbali mbali waliohudhuria mahafali hayo.


..............................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekiri kuwa Wizara, Idara na taasisi za Serikali zina matumizi madogo ya takwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini hali ambayo inachangia kurudisha nyuma shughuli za upangaji wa maendeleo za wananchi.

Makamu wa Rais wa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo trh 19-Nov-2016 katika hotuba yake kwenye mahafali ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Jijini Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, Idara na taasisi za Serikali kuimarisha matumizi ya takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga na kuweka mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Makamu wa Rais ameutaka uongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika uimarishe ushirikiano na Wakuu wa Takwimu wa Afrika kwa kuhakikisha watakwimu wanaoingia katika soko la ajira wanafanya kazi zao kwa kufuata misingi ya kisheria na kanuni zake katika ukokotoaji wa takwimu zinazokubalika kitaifa na kimataifa ambazo zitawezesha Afrika kupanga maendeleo ya wananchi kwa ufanisi mkubwa.

Amewahimiza wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika pindi watakapoanza kufanya kazi zao wafanye kazi kwa ufanisi na kwa umakini wa hali ya juu ili kutimiza azma ya kutokomeza kabisa umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 katika bara la Afrika.

“Wito wangu kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuhakikisha zinaimarisha vitengo vya takwimu kwa kuwaruhusu maofisa waliopo katika vitengo vyao vya sera na mipango wapate fursa ya kupatiwa mafunzo elekezi na ya muda mfupi kwa ajili ya kuongeza ujuzi wao wa kuchambua na kukokotoa takwimu rasmi”

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa hategemei kuona wahitimu walio maliza masomo yao katika ngazi mbalimbali katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wamalize soli za viatu kusaka ajira na kwamba Serikali itawawekea mazingira bora ya kupata ajira haraka.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema Serikali itaendelea kushirikiana kikamilifu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kutumia takwimu sahihi ambazo zimetolewa na ofisi hiyo katika kupanga shughuli za maendeleo za taifa.
Katika mahafali hiyo ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewatunuku vyeti wahitimu 133 katika ngazi za Shahada ya Uzamili ya Takwimu, Shahada ya awali ya takiwmu na Stashahada ya takwimu kwa wahitimu kutoka nchi Kumi za Afrika ambazo ni Nigeria,Ghana,Sierra Leon, Ethiopia,Somalia, Uganda, Swaziland, Liberia, Rwanda na mwenyeji Tanzania.


Washiriki wa Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani yaliyotaribiwa na Taasisi ya Doris Mollel wakiwa na bango lenye ujumbe wa kuadhimisha siku hiyo, iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Matembezi hayo yalianzia katika Uwanja wa Amani kupitia Uwanja wa Tumbaku na kuishia Viwanja vya Maisara.
 Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakijumuika pamoja Wadhamini na Waratibu wa Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, wakishiriki Matembezi hayo, yalianzia katika Uwanja wa Amani kupitia Uwanja wa Tumbaku na kuishia Viwanja vya Maisara, Mjini Unguja, Zanzibar.
Brass Band ya Chuo cha Mafunzo, Zanzibar ikiongoza Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Dunian,  iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Matembezi hayo yalianzia katika Uwanja wa Amani kupitia Uwanja wa Tumbaku na kuishia Viwanja vya Maisara.

Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akiwa pamoja na Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel pamoja na washiriki wengine katika Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yaliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Harusi Said Suleiman akitoa hotuba yake, katika hafla ya Kilele cha siku ya Mtoto Njiti Duniani, iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Vodacom ndio Wadhamini wakuu walioeza kufanyikisha shughuli hiyo. Kulia ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Mratibu wa Matembezi hayo, Doris Mollel na kushoto ni Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu.
Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akizungumza katika hafla ya Kilele cha siku ya Mtoto Njiti Duniani, iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Vodacom ndio Wadhamini wakuu walioeza kufanyikisha shughuli hiyo.

Baadhi ya Vikundi vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar, wakipasha moto misuli mara baada ya kumalizika kwa Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yaliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016.






Mshehereshaji wa hafla hiyo, Mishy Bomba akiweka sawa mambo.






Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akipokea


No comments :

Post a Comment