Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (katikati)
na viongozi wengine kutoka kushoto, Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Dkt.
Alexander Kyaruzi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt.
Juliana Palangyo,Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,
(Waziri Mkuu), Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, wakishangilia baada ya kukata utepe
kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha
cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya
usambazaji umeme katika jiji la Dar es
salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Novemba 16, 2016
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAZIRI
Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, amezindua kituo cha udhibiti na
usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es
Salaam, leo Novemba 16, 2016.
Kituo
hicho kipya na cha kisasa, kimejengwa kwa ufadhili wa serikali ya Norway na
Tanzania, chini ya mpango wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini.
“Serikali
ya awamu ya Tano, iliwaahidi Watanzania, wakati tukiomba kura, ya kwamba,
tutaboresha huduma ya umeme kote nchini, na leo hii ni ushahidi tosha
tunatekeleza kwa vitendo ahadi zetu.” Alisema Waziri Mkuu ambaye alimwakilisha
Rais wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Akimkaribisha
waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Profesa Sospeter Muhongo amesema,
watanzania wanahitaji umeme tena ulio bora, na sasa kituo hicho ni jawabu la
kuwapatia umeme ulio bora.
“Kati
ya vitu ambavyo sitarajii kuvisikia ni mgao wa umeme, lakini pia bei ya umeme, kuusu
bei tutakaa, pembeni na watu wa TANESCO kulizungumzia hili. “ Alitoa hakikisho
Waziri Muhongo.
Kwa
upande wake, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Mh. Kai Mykkanen, alisema,
teknolojia iliyotumika kwenye mitambo ya kituo hicho ni ya kisasa ijulikanayo
kama Distribution SCADA System, na
inauwezo wa kutambua hitilafu ya umeme kwa haraka na hivyo kurahisisha
kurekebisha hitilafu hiyo kwa wakati.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, alisema, Mradi wa
uboreshaji huduma za umeme jijini Dar es Salaam ulibuniwa kwa lengo la
kuboresha miundombinu ya umeme katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko
kubwa la mahitaji ya umeme katika sekta za kiuchumi hususan katika maeneo ya
katikati ya jiji, Kariakoo, Ilala na maeneo ya wilaya ya Kinondoni.
Alisema,
utekelezaji wa mradi huu umehusisha ujenzi wa kituo cha kupoza nguvu za umeme
chenye ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV cha City Centre, ujenzi wa mfumo wa
njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmission Line) na
kwa kutumia minara (Overhead Line) ya msongo wa wa kilovolti 132 kutoka kituo cha
Ilala hadi kituo cha City Centre umbali wa Kilomita 3.4, vile vile ujenzi wa
mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission
Line) kutoka kituo cha Makumbusho hadi kituo cha City Centre umbali wa kilomita
6.67.
“Mheshimiwa
Waziri Mkuu, kituo hiki ambacho kinajulikana kitaalamu kama Distribution SCADA System
kitawezaesha watoa huduma wetu kufuatilia kwa haraka zaidi pale matatizo ya
umeme yanapojitokeza kwa kutumia mifumo ya ksiasa ya kompyuta.” Alifafanua
Mhandisi Mramba na kuongeza.
“Nia
hasa ni kujenga vituo vingine kama hiki kwa kuanza na miji mingine mikubwa ya
Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma.” Alisema.
Waziri Mkuu na wageni wengine wakitembelea chumba cha mitambo yaudhibiti na
usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme Distribution SCADA System
Waziri Mkuu akitembeela moja ya mitambo inayopatikana kwenye kituo chicho (Server)
Mtaalam wa mitambo, wa shirika la Umeme
Nchini Tanzania, (TANESCO), Bi, Mwajua Turkey, kushoto, akimpatia
maelezo waziri mkuu wakati akitembelea kituo hicho muda mfupi kabla ya
kukizindua rasmi
Waziri Mkuu akitoa hotuba yake
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akitoa hotuba yake
Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Mh. Kai Mykkanen
Waziri Mkuu akipokelewa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowasili kwenye hafla hiyo
Waziri Mkuu akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Waziri Mkuu akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa
Waziri Mkuu akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo
Waziri Mkuu akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi
Waziri Mkuu akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba
Waziri Muhongo akizungumza na Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen
Waziri wa Bishara na Maendeleo wa
Finland, Kai Mykkanen, (kushoto) na Balozi wa Finland Nchini, Pekka
Hukka, (kulia), wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini, Dkt. Juliana Palangyo
Waziri Mkuu, akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi huo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, (wapili
kushoto), Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (wapili
kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana
Palangyo, (kushoto) na Waziri Kai(kulia), wakishangilia baada ya
uzinduzi
Meneja wa kituo cha udhibiti na
usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar es salaam, Mhandisi Alex P. Kalanje.(mwenye kipaza sauti), akitoa maelezo kwa waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom
Nyanduga akisisitiza jambo kwenye mkutano na wajumbe kutoka nchi za
Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
TUME
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeshukuru Umoja wa Mataifa
kwa msaada wake mkubwa inaotoa kwa taasisi zisizo za kiserikali za
kujengea uwezo wa kuweza kutetea haki za binadamu nchini Tanzania.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay wakati wajumbe
wa nchi za Nordic ambao ni wafadhili wakubwa wa programu za Umoja wa
Mataifa zinazotekelezwa nchini Tanzania walipozuru katika ofisi hizo kwa
mazungumzo.
“Kuna
ongezeko kubwa la ufahamu kuhusu haki za binadamu, upatikanaji wa haki
kwa makundi maalumu, uandishi wa habari kuhusu haki za binadamu na
kuboreshwa kwa huduma za kisheria na ukaribu wa serikali wa kufanyakazi
na wadau wa haki za binadamu,” alisema Massay akifafanua zaidi kuhusu
manufaa ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa katika kuboresha haki za
binadamu nchini.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom
Nyanduga (wa pili kushoto) akitoa neno la ukaribisho kwa wajumbe kutoka
nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa
Mataifa (hawapo pichani) ulipotembelea tume hiyo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Katibu
Mtendaji wa THBUB, Mary Massay (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Awa Dabo
(kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Katika
mazungumzo yao na ujumbe wa nchi za Nordic ambazo ni Sweden, Denmark,
Norway Finland na Iceland kulikuwepo pia asasi mbalimbali zisizo za
kiserikali kama Women’s Legal Aid Center, Tanzania Women Lawyers
Association, Tanzania Women Judges Association, Legal Aid and Human
Rights Center, Human Rights Defenders Coalition, na Tanganyika Law
Society.
Katika
mazungumzo hayo asasi hizo zilielezea ufanyaji kazi wao mafanikio na
changamoto wanazokumbana nazo na umuhimu wa ufadhili wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa.
Akizungumzia
changamoto zinazokabili Umoja wa Mataifa, serikali na asasi Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema ipo haja ya kuwa na muono wa
muda mrefu wa kuratibu shughuli zinazohusiana na maendeleo endelevu.
Katibu
Mtendaji wa THBUB, Mary Massay akizungumzia shughuli mbalimbali
zinazofanywa na tume hiyo kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana
na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani)
ulipotembelea tume hiyo.
Alisema
kwamba mabadiliko ya kitabia kwa binadamu huchukua muda mrefu
kukubalika hivyo ni wajibu wa kila mmoja kufanya bidii ya kuhakikisha
kwamba maisha yanabadilika na watu wanakumbatia mambo ya kisasa
yanayochochea maendeleo yao na jamii
Akizungumza
kwa niaba ya wajumbe kutoka nchi hizo za Nordic, Anders Rönquist,
ambaye ni kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la
Sweden (SIDA), alisema pamoja na changamoto zilizopo kitaasisi, kisiasa,
kifedha na kitamaduni maendeleo yaliyopo katika sheria na haki za
binadamu nchini Tanzania yanatia moyo sana.
Alisema
ipo haja ya serikali kuendelea kuhimiza mabadiliko na kwamba wao wapo
tayari kusaidia mkakati wa kuboresha masuala ya sheria na haki za
binadamu.
Kiongozi
wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA),
Anders Rönquist (kulia) akizungumza kwa niaba ya wajumbe kutoka nchi
hizo za Nordic ulipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Awa Dabo
(kulia), akizungumza katika mkutano huo ambapo alishukuru mataifa hayo
kwa kuendelea kusaidia programu za haki a binadamu nchini Tanzania.
Alisema kwamba haki za binadamu ni kitu cha msingi katika maendeleo kwa
kuwa hakuna maendeleo ya kweli bila kuwapo na haki za binadamu. Alisema
kwamba maendeleo na haki za binadamu ni mambo yanayoshabihiana na
kuimarika kwake kunasaidia kuimarisha ustawi wa jamii. Alishukuru pia
serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kwamna masuala ya utawala bora na
haki za binadamu yamo katika mpango wa miaka mitano wa maendeleo ambao
unasaidiwa pia na UNDAP ll.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom
Nyanduga akisisitiza jambo kwenye mkutano na wajumbe kutoka nchi za
Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC),
Theodosia Muhulo akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo
chake katika kuhakikishwa wanawake na watoto wapata msaada wa kisheria
wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na
wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mwansheria
kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Benedict Ishabakaki akizungumzia shughuli mbalimbali wanazofanya za
msaada wa kisheria wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic
walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
Jaji
wa Mahakama Kuu na Makamu Mwenyekiti wa TAWLA, Sophia Wambura
aki-'share' uzoefu wake katika masuala ya sheria wakati wa ziara ya
wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika
ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani kwa
Mwenyekiti wa THBUB wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic
walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
Jaji
wa Mahakama Kuu na Makamu Mwenyekiti wa TAWLA, Sophia Wambura
akikabidhi zawadi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia)
baada ya kumalizika mkutano wa wajumbe kutoka nchi za Nordic
walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
Jaji
Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Eusebia Munuo akikabidhi zawadi kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe.
Bahame Tom Nyanduga wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic
walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipokutana na uongozi wa ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Picha
juu na chini ni wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam
kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).
No comments :
Post a Comment